Mgombea
udiwani (Chadema) Kata ya Buhangaza, Mchungaji Athanasio Makoti (28)
aliyepotea Februari 2,2018 katika mazingira ya kutatanisha amepatikana
akiwa hajitambui.
Makoti
amepatikana leo Februari 5,2018 saa moja asubuhi, Katibu wa Chadema
wilayani Muleba, Elisha Kabombo alisema alitelekezwa na watu
wasiojulikana jirani na Hospitali ya Kagondo.
Amesema
wananchi waliokuwa wakipita eneo hilo usiku wa kuamkia leo walimuona
akiwa kando mwa barabara ya kuelekea Bukoba, hivyo kumpeleka hospitali.
“Hali yake si nzuri kwa sababu hawezi kuzungumza vyema wala kuketi. Kawekewa dripu za maji. Tuzidi kumuombea,” amesema.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Isack Msangi amethibitisha kupokea
taarifa za kupatikana mgombea huyo. Amesema vyombo vya dola vinamhoji
ili kuendelea na uchunguzi.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kagondo, Dk Humphrey Batungi alipoulizwa afya ya mgombea huyo amesema ni mapema kuzungumza.
“Ninaelekea
kwenye kikao nitafute mchana baada ya dawa anazotumia mgonjwa kufanya
kazi na huenda akawa na mabadiliko,” amesema Dk Batungi.
Katibu
wa uenezi wa Chadema jimbo la Muleba Kusini na mratibu wa chama hicho
jimbo la Muleba Kaskazini, Hamisi Yusufu amesema baada ya kufikishwa
hospitali alikutwa na majeraha, huku akizungumza kwa shida.
Amesema
mgombea huyo wa udiwani aliwaeleza amenyang’anywa fedha, waliomteka
walimfunga kitambaa cheusi usoni na kumtaka asigombee uchaguzi
utakaofanyika Februari 17,2018 na amekiri kuwafahamu baadhi ya
waliomteka.
Katika uchaguzi huo anachuana na mgombea wa CCM, Jenitha Tibeyenda na wa NCCR-Mageuzi, Grason Anaseti.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment