Monday, 20 June 2016

Uingereza kusalia Umoja wa Ulaya?

By: Unknown On: 00:00
  • Share The Gag
  • David Cameroon , waziri mkuu wa Uingereza
    Leo BBC inaanza msururu wa ripoti tulizokuandalia kuelekea kura ya maoni ya Uingereza Alhamisi hii itakayo amua iwapo taifa hilo lijitoe au lisalie katika Umoja wa Ulaya.

    Kampeni ya kura ya maoni nchini Uingereza na mijadala ya ama isalie kuwa mwanachama wa umoja wa ulaya ama lah,zoezi hilo lilizorota na kusababisha shughuli nyingi kusimama kufuatia mauaji ya Mbunge wa chama cha Labour, Jo Cox yaliyotukia Alhamisi iliyopita.
    Huku siku tatu zikiwa zimesalia kufikia siku ya upigaji wa kura ya maoni ,huku wapiga kura walio wengi wakiwa hawana maamuzi juu ya kura yao itaangukia wapi.

    Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, aliahidi wakati wa kampeni yake katika uchaguzi mkuu nchini humo kutetea kiti chake mwaka 2015 kwamba endapo atashinda,serikali yake itaruhusu kura ya maoni ipigwe ili kuwapa nafasi jumuiya ya Waingereza fursa ya kuamua mustakabali wa baadaye wa taifa hilo katika Umoja wa ulaya

    Chanzo BBC.

    Sunday, 19 June 2016

    Muhogo wa kuchemsha waua watatu Morogoro

    By: Unknown On: 23:58
  • Share The Gag

  • Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.   
    WATU watatu wamekufa mkoani Morogoro na wengine wawili kunusurika kifo, kutokana na kula muhogo wa kuchemsha unaosadikiwa una sumu. Kati ya waliofariki kwa kula muhogo unaosadikiwa kuwa una sumu, wawili ni pacha wakati na wengine wawili wamenusurika na mmoja akiwa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.

    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema hayo jana ofisini kwake kuwa tukio la kula muhogo unaosadikiwa kuwa na sumu lilitokea Juni 18, mwaka huu saa 9 alasiri kata ya Kauzeni Manispaa ya Morogoro.
    Matei alitaja waliofariki katika tukio hilo ni Omary Mohamed aliyefariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitalini wakati pacha wake Hamis Mohamed alifariki baada ya kufikishwa hospitalini hapo.
    Alitaja mwingine aliyefariki ni Daud Herman (31), mkazi wa Kauzeni aliyefariki akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ya Mzinga iliyopo Manispaa ya Morogoro.

    Kamanda huyo alisema watu hao walifikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro baada ya hali zao kuwa mbaya kutokana na kuwa miongoni mwa watu watano waliokula muhogo huo, ambao wawili walinusurika baada ya kupatiwa matibabu.
    Alitaja walionusurika kifo ni Amos Kunambi (30), mkazi wa Kauzeni aliyetibiwa na kuruhusiwa baada ya hali yake kuwa nzuri wakati Joshua Msiani (24) anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa.
    Alisema miili ya marehemu hao watatu, imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa, huku uchunguzi wa kitabibu ukiendelea ili kubaini uhalisia wa ukweli juu ya muhogo huo kuwa na sumu.

    Mmoja wa manusura Joshua Msiani aliwaambia waandishi wa habari hospitalini jana kuwa akiwa na wenzake watano, walikuwa wakifyatua matofali eneo la kata ya Kauzeni Manispaa ya Morogoro.
    Msiani alisema akiwa eneo hilo, wenzake walileta muhogo na kumkaribisha kula, ingawa aliwajibu kuwa ameshiba lakini walizidi kumlazimisha ili kula muhogo huo wa kuchemsha. “Nikaona wananilaumu sana, ikabidi nichukue kipande kimoja nikala, na ndipo muda mchache nikapoteza fahamu hadi nilipokuja kuzinduka nikiwa hospitalini Mzinga,” alisema.

    Katika tukio jingine, watu wawili wa familia moja wamekufa baada ya mmoja wao anayesadikiwa kuwa na ugonjwa wa akili, kumchoma na mkuki tumboni mdogo wake, Raymond Melikioni na kufa papo hapo Juni 17, mwaka huu tarafa ya Mgeta wilaya ya Mvomero.

    Chanzo HabariLeo.

    Donald Trump azungumzia uhalifu

    By: Unknown On: 23:55
  • Share The Gag
  • Donald Trump
    Mgombea anayepewa nafasi kubwa ya kupeperusha bendera ya Republican katika kinyanganyiro cha urais huko Marekani Donald Trump amesema muda umefika kwa nchi hiyo kutafakari kwa kina juu ya matumizi ya taarifa binafsi za watu katika harakati za kupambana na uhalifu.

    Bwana Trump aliyasema hayo katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha habari za CBS akijaliana juu ya mpango wa siku za usoni wa taifa hilo,kufuatia mauaji yanayokithiri nchini humo, na hasa la hivi karibuni katika klabu moja ya usiku mjini Orlando yaliyojiri wiki iliyopita.

    Ameongeza kusema kwamba nchi zingine zimetumia mbinu tata za rangi ya mtu , dini, utaifa au ukabila kama mbinu ya kutambua nani anaweza kufanya uhalifu.

    Chanzo BBC.

    Thursday, 16 June 2016

    Mwili wa mvulana aliyenyakuliwa na mamba wapatikana

    By: Unknown On: 05:01
  • Share The Gag
  • Mamba
    Maafisa wa polisi waliokuwa wakiutafuta mwili wa mvulana wa miaka 2 aliyenyakuliwa na mamba katika bustani ya shirika la Walt Disney World mjini Florida wameupata mwili wake.

    Waogeleaji waliupata mwili huo ambao ulikuwa hauna majeraha yoyote na wanaamini ni ule wa mvulana huyo wa miaka miwili ambaye alinyakulwia na mamba na kuingizwa ndani ya maji siku ya Jumanne jioni mbele ya familia yake.

    Mkuu wa kaunty ya Orange Jerry Demings amesema kuwa jina la mvulana aliyetoweka na mamba huyo ni Lane Graves kutoka Nebraska.
    Tangu shambulio hilo mamba watano walikamatwa na kuuawa kwa lengo la kutafuta mabaki ya mwili wa kijana huyo.

    Mwili uliopatikana majini bado haujatambuliwa rasmi lakini maafisa wa polisi wana imani ni ule wa Lane.
    Mapema siku ya Jumatano maafisa wa polisi walisema kuwa hakuna tashwishi kwamba mvulana huyo alifariki.

    Chanzo BBC.

    Ni halali wapenzi wa jinsia moja kuchunguzwa kimatibabu Kenya

    By: Unknown On: 04:58
  • Share The Gag
  • Wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya
    Mahakama moja nchini Kenya imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyokuwa ikipinga uhalali wa uchunguzi wa tupu ya nyuma kama idhibati ya ngono ya wapenzi wa jinsia moja.

    Mahakama kuu ya Mombasa imesema kuna sheria fulani nchini Kenya inayohalalisha uchunguzi kama huo kwa sababu za kutafuta ushahidi. Kwenye uamuzi wake, hakimu Mathew Emukule alisema kulikuwa na ruhusa fulani kwenye sheria za Kenya kuchunguza maumbile ya binadamu kwa lengo la kutafuta ushahidi wa hatia kama unajisi au kuficha madawa ya kulevya.
    Aidha alitupilia mbali wazo kuwa uchunguzi kama huo unabagua kijinsia, akisema kuwa tupu ya nyuma si ya kijinsia bali ni ya utumbo. Aidha alisema uchuguzi kama huo ulikubalika kwani walalamishi walikubali kufanyiwa.

    Hatua hiyo inajiri baada ya wanaume wawili kuwasilisha ombi la kikatiba wakisema walifanyishwa uchunguzi wa kimaumbile sawa na virusi vya ukimwi na hepatitis, walipokamatwa kwa shutma za mapenzi ya jinsia moja mnamo Februari mwaka jana.
    Mapenzi ya jinsia moja ni hatia nchini Kenya, na adhabu yake ni kifungo gerezani kwa muda usiozidi miaka kumi na nne.

    Chanzo BBC.

    Ufisadi Bodi mikopo ya wanafunzi Tanzania

    By: Unknown On: 04:54
  • Share The Gag
  • Profesa Joyce Ndalichako 

    Ripoti ya uchunguzi wa kamati iliyoundwa na Waziri Elimu wa Tanzania Profesa Joyce Ndalichako imeibua ufisadi katika bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini Tanzania.
    Ufisadi huo ni pamoja na bodi kutoa mikopo isiyojulikana kwa wanafunzi zaidi 2000 wa kiasi cha shilingi bilion 14 za Tanzania sawa na dola milioni 7 za marekani.

    Kamati hiyo iliundwa baada ya kusimamishwa kwa watendaji wakuu wa bodi hiyo.
    Aidha bodi hiyo imegundua upotevu wa Zaidi ya dola Milioni 1.3 zilizolipwa kwa wanafunzi wa vyuo kadhaa ambazo hazitambuliwi na vyuo hivyo huku fedha hizo zikiwa hazijarudishwa.
    Waziri huyo amesema kuwa baada ya kuyabaini mambo hayo,serikali serikali imechukua hatua za kutoa wiki mbili kwa bodi ya mikopo kuwachukulia hatua mara moja wote wanaohusika ikiwemo watumishi waliosimamishwa.
    February mwaka huu waziri huyo aliwasimamisha kazi baadhi ya watendaji wakuu wa bodi hiyo baada ya kubaini udhaifu katika utekelezaji wa majukumu yake ambapo pia ameagiza uchungu ufanyike

    Chanzo BBC.



    Afrika Kusini yaadhimisha maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi

    By: Unknown On: 04:52
  • Share The Gag
  • Afrika kusini
    Afrika Kusini inaadhimisha miaka 40 tangu maandamano ya wanafunzi wa Soweto, walipopinga ubaguzi wa rangi katika elimu kwa kulazimishwa kusomeshwa kwa lugha ya Ki-Afrikaan.
    Mamia ya wanafunzi walifariki katika vurugu zilizojiri wakati serikali ya ukoloni ya wazungu makaburu ilipotumia nguvu kupita kiasi, kujaribu kuzima maandamano hayo.
    Maandamano hayo yalikuwa kama mwanzo wa kuelekea hatua za kumalizwa kwa utawala wa makaburu wa Afrika Kusini.
    Makamu wa rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa, ameweka shada la maua kwenye kaburi la kijana Hector Pietersen.
    Afrika Kusini Ni picha ya mwili wa kijana huyo uliokuwa unabebwa na mwanafunzi mwenzake baada ya kupigwa risasi na polisi.
    Picha hiyo ilibua hamasa na hasira kubwa na kuufanya ulimwengu kulaani ukatili uliokuwa ukiendelezwa na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo.

    Chanzo BBC.