Saturday, 7 January 2017

Lowassa Atema Cheche Arusha

By: Unknown On: 23:15
  • Share The Gag
  • Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayotokea duniani katika kipindi hiki hayawezi kuzuiliwa na mifumo iliyopo.

    Akizungumza jana na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Mateves katika Halmashauri ya Arusha Vijijini, Lowassa alisema nguvu kubwa ya mabadiliko inayoonyeshwa na Chadema itawaletea wananchi maendeleo.

    Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, chama chake kilipata kura nyingi kwenye maeneo mengi licha ya kutokuwa washindi na kwamba wamejipanga katika uchaguzi wowote utakaofanyika kuhakikisha kinashinda kwa kishindo.

    “Ninazindua kampeni za uchaguzi huu mdogo nikiwa na imani kubwa kwa Chadema. Nina imani kuwa mgombea wa chama hiki atatekeleza anayoyaahidi na kuondoa kero zenu na ndiyo maana Chadema inaungwa mkono zaidi nchini,” alisema Lowassa.

    Alisema katika mpango wa kukiimarisha chama hicho, wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema wanazunguka nchi nzima kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa.

    Katika harakati za kuhakikisha kwamba upinzani unaibuka na ushindi katika chaguzi ndogo zote zilizopangwa kufanyika Januari 22, Lowassa alisema leo atakuwa Zanzibar katika uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa Dimani kwa tiketi ya CUF, Abdulrazaq Khatib Ramadhan na baada ya hapo ataelekea Bukoba katika kampeni za Ukawa.

    Uchaguzi wa Kata ya Mateves unafanyika baada ya Mahakama kuagiza urudiwe kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi ulipita ambao mgombea wa CCM alitangazwa mshindi.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Rushwa ya ngono bado tishio nchini

    By: Unknown On: 23:13
  • Share The Gag
  • Makamu wa Raisi Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nane wa majaji ulioandaliwa na Chama Cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), unaofanyika kila baada ya miaka miwili. Mkutano wa mwaka huu uliokuwa na kauli mbiu isemayo ‘Kuongoza njia kufikia hitaji la upatikaji wa haki kwa wote na kwa wakati.

    SUALA la rushwa ya ngono limeendelea kuwa tishio nchini hadi kusababisha wanawake wengi kujiengua katika nafasi zao.
    Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati akifungua Mkutano wa Nane wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), uliofanyika Dar es Salaam jana.
    Samia alisema ni jambo la kuvunja moyo, kuona kwamba katika Karne ya 21 suala la rushwa ya ngono, linaendelea na kusababisha wanawake wengi kujiengua katika nafasi zao.

    Makamu wa Rais alionya juu ya vitendo hivyo vya rushwa ya ngono, vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wenye madaraka na kusema tabia hiyo ni mbaya na lazima ikomeshwe mara moja katika jamii.
    “Matumaini, matarajio na ndoto za wanawake, zimekuwa zikikatishwa na watu wachache ambao ni hatarishi, hivyo tunahitaji kufanya kazi kuhakikisha kwamba tunawasaidia kwa hali na mali kwa sababu wahanga hao wanaweza kuwa mama yako, dada, mke na binti yako,’’ alisema Makamu wa Rais.
    Alisema kuwa vitendo hivyo vya rushwa ya ngono, huzuia na kukwamisha juhudi za wanawake kufikia huduma za kijamii na za kiserikali ipasavyo, ikiwemo elimu, ajira na haki kwa ajili ya ustawi wa wanawake.
    Makamu wa Rais aliwaagiza majaji na mahakimu wanawake kote nchini, kupambana ipasavyo na kukabili vitendo vya unyanyasaji kijinsia na rushwa ya ngono ili kusaidia wanawake kupata haki zao za msingi bila kubaguliwa katika jamii.

    Alisisitiza kuwa atahakikisha kwamba wanawake na watoto, wanapatiwa haki zao kwa uhuru bila ya ubaguzi wala vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi yao.
    Samia aliongeza kuwa kuondoa vikwazo vya kisheria kuhusu ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake ni miongoni mwa maeneo makubwa sita katika kuondoa pengo kubwa la kiuchumi.
    Alifafanua kuwa serikali inahamasisha kushiriki kutekeleza sheria za kimataifa katika kupambana na unyanyasaji wa kijinsia, rushwa ya ngono na umiliki wa mali dhidi ya wanawake. Samia aliwahimiza majaji hao kutoa hukumu kwa wakati katika kesi wanazoendesha ikiwa ni pamoja na kufuata maadili na kanuni zilizowekwa.
    Aidha, aliwataka kuhakikisha kwamba wanatoa bure elimu ya haki za binadamu na ujuzi kwa maofisa wa mahakama, watunga sera na waathirika wa ukatili wa kijinsia. Akitoa takwimu za ushiriki wa wanawake katika nafasi mbalimbali, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman alisema asilimia 44 ya majaji waliopo katika mahakama ni wanawake huku Mahakama Kuu pekee ikiwa na asilimia 47.9 ya wanawake.

    Alisema Bunge lina asilimia 46.6 ya wanawake wakati katika nchi jirani ikiwemo Kenya, wana idadi ndogo ya majaji wanawake ambayo ni asilimia 3.3. Jaji Othman alisema kuwa wasajili wa mahakama waliopo, asilimia 34 ni wanawake na kwamba nafasi ya uongozi hususan kwa mahakimu wafawidhi wa mahakama za mwanzo na kati, imeongezeka.
    ‘’ Malengo yetu kama mahakama ni kuongeza idadi ya wanawake katika mahakama zetu zote, kwani ndio mahitaji na matakwa ya sheria. Pia niipongeze TAWJA ambayo imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika mahakama kwa kutoa elimu kuhusu masuala ya kisheria kwa maofisa wa mahakama na wengine wenye uhitaji,’’ alisema Jaji Othman.

    Aidha, alisema kuwa kuongeza idadi ya mahakama za mwanzo na za kati ni ishara ya kuongeza huduma za kisheria pamoja na utoaji wa elimu, itakayosaidia kuiboresha mahakama pia.
    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAWJA, Jaji Imani Aboud alisema kuwa mkutano huo umekuwa ukifanyika kila mwaka na lengo ni kuzungumzia masuala mbalimbali, ikiwemo mafanikio, changamoto na malengo yao ya baadae.
    Alisema kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili ni pamoja na rushwa ya ngono, ambayo licha ya mwanamke kuwa na haki ya kupata kazi, huombwa rushwa hiyo ili kumrahisishia upatikanaji wake.
    ‘’Tumejipanga kufanya kazi kwa mujibu wa sheria pamoja na kutoa elimu kuhusu sheria zilizopo na kuwasaidia wanawake na jamii kwa ujumla, kazi hii itafanyika kwa kadri serikali ya awamu hii inavyotaka,’’ alisema Jaji Aboud.

    Chanzo HabariLeo.

    Kocha wa Azam Ameitaja Sehemu Alipoikamata Yanga

    By: Unknown On: 23:06
  • Share The Gag


  • Yanga wanategemea sana mipira ya pembeni, sasa tulijaribu kuangalia watu wanaowachezesha wale watu wa pembeni, tukawakamata na ukiwakamata Yanga kwenye midfield basi unakuwa umeua plan zao wakaishiwa maarifa wakawa hawajui nini cha kufanya sisi tukawa tunatengeneza nafasi na kuzitumia,” anasema kocha wa muda wa Azam Idd Cheche baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi wa kihistoria dhidi ya Yanga.

    Kwenye michezo miwili iliyopita Azam haikuonesha kiwango kizuri kiuchezaji huku washambuliaji wake wakishindwa kutumia vizuri nafasi, Cheche amesema tatizo lilikuwa ni umaliziaji na walilifanyia marekebisho ndio maana safu ya ushambuliaji ilikuwa hatari dhidi ya Yanga.

    “Tumerekebisha safu ya shambuliaji ndio ilikuwa inasumbua kidogo, tulikuwa tunapata nafasi lakini tuikuwa tunashindwa kuzitumia, movements zilikuwa ndogo kwa hiyo tumelifanyia kazi hili suala la finishing ndio limeleta haya matunda yaliyotokea.”

    Azam imefuzu hatua ya nusu fainali na inatarajia kukutana na timu itakayomaliza nafasi ya pili kutoka Kundi A lenye timu za Simba, Taifa Jang’ombe, Jang’ombe Boys na URA ambazo zote zina nafasi.

    Hii ndio kauli ya Cheche kuelekea mechi ya nusu fainali: “Yoyote atakaekuja kwenye nusu fainali atakuwa ni mzuri na sisi tumejiandaa kupambana nae tuhakikishe tunavuka tunaingia fainali na kuchukua kombe.”

    Credit; Udaku Special

    Diamond kufunika ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2017’

    By: Unknown On: 23:05
  • Share The Gag
  • Ule wimbo unaosikika mtaani wa ‘pesa kupotea mifukoni’ haumhusu Bosi wa WCB, Diamond Platinumz anayeendelea kuzihesabu ‘deals’ kubwa zaidi za matukio ambayo dunia nzima inayaangalia kwa macho yote.

    Siku chache baada ya kutumbuiza kwa ustadi mkubwa kwenye tuzo za CAF jijini Abuja nchini Nigeria, Diamond amealikwa kutumbuiza kwenye ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Africa 2017 (AFCON 2017), Januari 14 nchini Gabon.

    Chibu Dangote amewapa habari hiyo njema mashabiki wake kupitia mitandao ya twitter na Instagram, kwa kupost taarifa ya show yake hiyo iliyowekwa kwenye akaunti maalum ya AFCON 2017.

    “GABON!!! You know we gat to make a World History on the 14th January right?? See you this this Coming Weekend then…👈 #WcbWasafi” aliandika.

    Ingawa Tanzania haipo miongoni mwa nchi zinazoshiriki kombe hilo kubwa zaidi la soka barani Afrika, mwaka huu bendera itapeperushwa kupitia tasnia ya Muziki na kuiacha alama ya Tanzania kwenye mashindano hayo.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Sunday, 1 January 2017

    Rais Magufuli kufanya ziara ya siku mbili kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera 1 january 2017

    By: Unknown On: 05:21
  • Share The Gag
  • Ikiwa imepita miezi mitatu na siku kadhaa toka kutokea kwa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera leo Rais wa Jamhuri wa Muungano Mh. John Pombe Magufuli anategemewa kuwasili mkoani humo kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kuwatembelea wananchi walioathirika na tetemeko la Ardhi lakini pia kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi kadhaa ya maendeleo ambayo yaliathiriwa kutokana na tetemeko hilo mkoani humo.

    Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mstapha jana alisema Rais ataingia asubuhi ya leo akitokea Geita na baadaye atahudhuria ibada ya misa na kesho yake ndiyo atawatembelea baadhi ya wananchi waliotumia nguvu zao kujenga nyumba zao na makazi baada ya kuharibiwa na tetemeko la Ardhi kisha atatembelea miradi ya ujenzi wa shule ya Sekondari ua Ihungo na kuweka jiwe la msingi na kuzungumza na wananchi.


    ==

    Credit;  Mpekuzi Blog 

    MFANYABIASHARA Ampiga Mwanafunzi Risasi ya Kichwa...Wananchi Wachoma Lori Lake

    By: Unknown On: 05:18
  • Share The Gag


  • MFANYABIASHARA Robert Mwikwabe, maarufu kama Ndugu, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga risasi ya kichwani na kusababishia kifo papo hapo mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari Sirari, Masaite Mrimi(17).

    Kutokana na tukio hilo, Mwikwabe ambaye pia ni mmliki Hoteli katika mji mdogo wa Sirari wilayani Tarime mkoani Mara, alinusurika kuteketezwa yeye na familia yake Hali hiyo ilitokea baada ya wananchi kuamua kuchoma moto lori la mfanyabiashara hiyo na kwenda nyumbani kutaka kuchoma hoteli.

    Mashuhuda walisema tukio hilo ni la juzi mchana, jirani na nyumba anayoishi mwanafunzi huyo, eneo la stendi mpya ya mabasi na malori ya Ngerengere.

    Walisema mfanyabiashara huyo alifika akiwa na lori lake likiwa na mawe na alisimama na kutaka kuchukua pumba za mchele, zilizomwagwa na malori yanayosafirisha ng’ombe kwenda nchini Kenya.

    Eneo hilo ni jirani na nyumbani kwao marehemu, ambako kulitokea mzozo kati ya Robert na wazazi wa mwanafunzi huyo. Kufuatia mzozo huo, mwanafunzi huyo aliyekuwa na panga mkononi, alimtishia kumkata Robert, ambaye alichomoa silaha yake aina ya bastola na kumpiga risasi kichwani na kumsababisha kifo.

    Baada ya tukio hilo, familia ya marehemu na wananchi walianza kumfukuza Robert aliyeacha lori lake likiwa na mawe na kukimbilia lori lake lingine la jirani. Kisha alikimbilia Kituo cha Polisi Sirari, kuokoa maisha yake.

    Umati mkubwa wa watu kutoka vijiji vya Ngerengere na Sirari, walikwenda nyumbani kwa mfanyabiashara huyo kwa lengo la kutaka kuchoma moto hoteli na nyumba.

    Lakini, polisi na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga walifanya juhudi kubwa kuwazuia wananchi hasa vijana, kuacha kuteketeza mali za mfanyabiashara huyo yakiwemo magari, ambayo sasa yamehifadhiwa kituo cha polisi kwa ajili ya usalama.

    Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Tarime-Rorya, Andrew Satta alithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafunzi huyo na kwamba maiti imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya Tarime.

    Credit; Udaku

    Picha: Rais Magufuli Ashiriki Ibada Ya Jumapili Ya Mwaka Mpya Katika Kanisa Kuu La Katoliki Jimbo La Bukoba Mkoani Kagera

    By: Unknown On: 04:46
  • Share The Gag
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibusu mkono wa Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya Ibada.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea katika katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kuwasili na kupokewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma (katikati) pamoja na Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini wa kwanza (kulia).
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya mwaka mpya katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya Ibada.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya Ibada.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kaburi la Marehemu Kadinali Rugambwa mara baada ya Ibada kanisani hapo.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya kushiriki Misa ya Mwaka mpya kanisani hapo. Katikati ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni Kanisani hapo.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma kushoto pamoja na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.



    ==

    Credit; Mpekuzi Blog