Mbunge
wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Msukuma amefunguka na kusema kuwa Rais
Magufuli hausiki katika sakata la kuvunja mkataba ambao umepelekea ndege
ya Tanzania Bombadier Q-400 Dash 8 kushikiliwa nchini Canada na kusema
wapinzani wanatafuta kiki.
Mbunge
Msukuma amesema kwa upeo wake jinsi alivyosikiliza upande wa upinzani
na majibu ya serikali anaona wazi kuwa ni kweli baadhi ya wapinzani wa
nchii hii wanahusika katika kukwamisha jambo hilo kama ambavyo serikali
ilivyosema na kudai Rais Magufuli hausiki katika jambo hilo.
"Binafsi
yangu naamini kabisa majibu ya serikali kuwa hili suala linauchochezi
wa wanasiasa, kwanza vitu vingi walivyosema wapinzani kuhusu sakata hili
la ndege ni vya uongo ukianzia lile suala la kuwa Rais Magufuli amekuwa
akiiitia hasara serikali hii.
"Tatizo
lililopo mahakamani la kampuni inayodaiwa kuishtaki Tanzania kampuni
hiyo imefanya kazi mwaka 1998-99 wakati Magufuli hakuwa Rais wa
Tanzania" alisema Mbunge Msukuma
Aidha
Mbunge huyo aliendelea kudai jumla ya deni la bilioni 87 ambayo
serikali ya Tanzania inadaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering
Ltd kwa kuvunja mkataba wa kazi halijatokana na serikali ya awamu ya
tano ya Rais John Pombe Magufuli.
"Deni
hili siyo kwamba limetokana na uongozi wa serikali ya awamu ya tano
lakini kama Rais huwezi kukataa deni ambalo serikali inadaiwa akiwa
madarakani lakini pia suala hili lipo mahakamani na hatua iliyofikia ni
hatua ya mwanzo kabisaa, na si kweli kwamba ndege imekamatwa unaweza
kuingia mitandaoni ukaiona ndege ilipo, bado ipo kwao hao Bombadier
hivyo Tundu Lissu anaposema ndege imekamatwa siyo kweli.
"Hao
watu hao wanaotudai wameenda kufile kesi ya kuzuia mali za Tanzania
zisiondoke na serikali inaweza kutoa utetezi wake kwa hiyo hili suala ni
kama linawekwa udalali na yote yanafanyika kutokana na umakini wa
serikali ya awamu ya tano kwa hiyo wapinzani wanatafuta kiki tu" alisisitiza Msukuma
Siku
ya Jumamosi ya tarehe 19 Agosti serikali ilikiri wazi kuwa ni kweli
kuna mgogoro uliopelekea ndege hiyo kushindwa kuingia nchini Tanzania
mwezi Julai kama ambavyo ilitangazwa awali na kusema serikali imeanza
kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inamaliza mgogoro huo.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment