Thursday, 30 June 2016

Mahakamani Kisutu: Watatu Mikononi Mwa Polisi Kwa Kubeba Mabango ya Kumkashifu Mtukufu Rais Magufuli

By: Unknown On: 22:53
  • Share The Gag

  • Jana wafuasi wa UKAWA walitiwa mbaroni baada ya kutoke mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kumkashifu Mtukufu Mkuu sana, Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

    Baadhi ya Mabango yalikuwa yanasomeka...

    Dikteta uchwara utashindwa
    Dikteta uchwara nenda Burundi

    Maoni Yangu;
    Kuna msemo usemao Delegatus Non Potest Delegare wakimaanisha la kujitakia halina majuto. Hawa wafuasi naona wamejitakia au wametumwa na viongozi wao uchwara kubeba mabango ya kashfa kwa Rais. Mbowe alikuwepo mahakamani, kwanini yeye hakubeba bango la kashfa? Kwanini awatumie wafuasi wachache wasiojielewa?

    Hivi nalo hili mtalalamika kuonewa?
    Kwanini hamuheshimu Taasisi ya Urais?
    Kwanini hamuheshimu Rais?

    Mnataka nini hasa wana wa upinzani?

    Crrdit; UDAKU SPECIAL

    Jeshi la Polisi Lapewa Siku 90 Kuhakikisha Mitambo ya LUGUMI Inafanya Kazi Vituo Vyote

    By: Unknown On: 22:51
  • Share The Gag

  • Jana akihitimisha bunge, naibu spika ametolea ufafanuzi utekelezaji wa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa alama za vidole(AFIS), hoja iliyojengwa kutokana na mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG) kwa kutokamilika kwa mradi huo.

    Agizo la bunge lilimtaka afisa masuhuli wa jeshi la polisi kuhakikisha mfumo wa AFIS unafanya kazi ndani ya kipindi cha miezi sita. Ripoti ilieleza mfumo wa AFIS ulikuwa unafanya kazi katika vituo 14 pekee kati ya vituo 108 hivyo agizo la kamati halikuwa limetekelezwa kikamilifu.

    Spika ametoa agizo kwa serikali kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi ndani ya miezi mitatu ili kuboresha uwezo wa jeshi la polisi kuwa na utambuzi wa haraka wa wahusika wa matukio ya kihalifu katika vituo vyote nchini. Pili masuala yote yaliyobainika kuwa na dosari za kiutendaji yapatiwe ufumbuzi haraka.

    Spika anatarajia sasa suala hilo litafikia mwisho na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali atafunga hoja yake baada ya kujiridhisha na utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.



    Credit;UDAKU SPECIAL 

    Shilole Kutafuta Mume Kijijini

    By: Unknown On: 22:48
  • Share The Gag

  • MKALI wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amejutia kuwapenda wanaume wa mjini kuwa ni wavivu kila sekta hivyo anajipanga kwenda kijijini kwao Igunga,Tabora kutafuta mume.

    Akistorisha na Showbiz Xtra, Shilole alisema kuwa, hataki tena kujichosha akili kwa wanaume wa mjini kwa vile ni wavivu bora aende Igunga kumpata mwanaume atakayeweza kufanya kazi kutokana na vyakula asili anavyokula.

    “Wanaume wa mjini wamezoea chipsi mayai, hawawezi chochote bora wa kijijini wanakula dona na wana akili za kufikiria,” alisema Shilole.

    Shilole alikuwa akitoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda.

    Credit;UDAKU SPECIAL

    Ungereza na mikataba mipya kibiashara

    By: Unknown On: 22:46
  • Share The Gag
  • Uingereza inaweza kuanza majadiliano ya mikataba mipya ya kibiashara iwapo tu itakuwa imejitoa kabisa katika umoja huo.
    Kamishina wa biashara wa umoja wa ulaya Cecilia Malmström amesema Uingereza inaweza kuanza majadiliano ya mikataba mipya ya kibiashara iwapo tu itakuwa imejitoa kabisa katika umoja huo.
    Katika mahojiano na BBC amesema kuna aina mbili za majadiliano ya utekelezaji wa makubaliano hayo.
    "Uhusiano kati yetu na uingereza kwa siku zijazo hautajadiliwa chini ya kifungu cha 50,ambacho ndicho kigezo cha kujitoa.
    Hivyo kuna aina mbili tu za majadiliano,moja unajitoa,kisha unajadiliana namna mpya ya uhusiano,au vyovyote inavyokuwa"
    Bi.Malmstrom ameongeza kuwa mpaka mikataba hiyo isainiwe ndipo biashara inaweza kufanyika chini ya taasisi ya kimataifa ya kibiashara.

    Chanzo BBC.

    Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika

    By: Unknown On: 22:23
  • Share The Gag
  • MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) hatimaye wametaja mfanyabiashara ambaye alibainishwa na Rais John Magufuli katika hafla ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Ikulu Dar es Salaam juzi.

    Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola alimtaja mfanyabiashara huyo kuwa ni Mohammed Mustafa Yusuf Ali anayetuhumiwa kuiibia Serikali matrilioni ya shilingi kwa kutumia mashine za kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na TRA na kutoa risiti bandia.

    Alisema TRA kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi ili kubaini makampuni yote yanayojihusisha na udanganyifu huu, ambapo hadi sasa jumla ya makampuni manne yamebainika kujihusisha na ukwepaji kodi kwa mtindo huu kuanzia mwaka 2010 hadi 2014; na jumla ya Sh 29,216,900,301.7 imebainika kutokulipwa serikalini na makampuni hayo kwa kipindi hicho.

    Alisema kwa sasa wanaendelea na mahojiano naye zaidi ili kuwabaini wote wanaohusika na mfumo huo na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

    Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa TRA, Alfayo Kidata aliyeambatana na Mlowola katika mkutano huo wa waandishi wa habari, makampuni hayo yamekuwa yakinunua risiti za manunuzi bandia kutoka kwa watu wanaomiliki mashine za EFDs ambazo hazijasajiliwa.

    “Makampuni hayo wakishanunua risiti za manunuzi bandia, hatimaye huzitumia risiti hizo kudai marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) bila kuwepo na bidhaa au huduma halisi iliyouzwa au kutolewa na mhusika, kitendo ambacho kinainyima serikali mapato stahiki kwa mujibu wa sheria,” alisema.

    Aliyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na Skol Building Material Ltd ambayo tangu mwaka 2012 hadi 2013 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 5,464,915,963 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya Sh 10,960,787,861 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 16,425,703,824 kwa kipindi hicho.

    Kampuni nyingine ni Farm Plant (T) Limited ambayo tangu mwaka 2010 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 5,930,170,573 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 4,948,393,516 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 10,878,564,089.

    Pia imo kampuni ya A.M.Steel & Iron Mills Limited ambayo kuanzia mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 79,016,112 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 131,693,518 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 210,709,630.

    Kampuni nyingine ni A.M Trailer Manufacturers Limited ambayo tangu mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa VAT ya Sh 638,221,034.80 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 1,063,701,724. 00 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 1,701,922,758.00.

    Alisema baada ya kubaini ukwepaji kodi huo kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo na mara baada ya uchunguzi kukamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kukwepa kodi.

    Alitoa mwito kwa wafanyabiashara wote kutojihusisha na kununua risiti za bandia na kudai marejesho ya VAT yasiyostahili kwa kuwa mamlaka imejizatiti kuendelea kuwabaini wafanyabiashara wanaokwepa kodi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa hatua stahiki.

    Aidha alisema uchunguzi wa awali pia umebaini kuwepo makampuni hewa 228 na kusisitiza kwamba wameusimamisha mfumo huo bandia na kutoa siku tatu kwa kampuni zote zinazodaiwa kulipa fedha hizo.

    “Hakuna yeyote anayekwepa kodi atasalimika, wote ni lazima walipe na sasa tumedhibiti mfumo huo bandia,” alisema.

    Juzi Magufuli akizungumza na Ma RC na Ma DC wapya, aliwataka wakasimamie vyema mapato katika maeneo yao kwani kumekuwepo na baadhi ya watu wajanja wanaotumia vibaya taasisi za Serikali ikiwemo Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brela) TRA kujinufaisha wenyewe na kuliingizia taifa hasara.

    Alisema: “Tulikuwa tunafuatilia mashine za EFDs zinazokusanya mapato, yupo mtu mmoja alitengeneza kampuni nyingi zilizokuwa zikimlipa asilimia tano ya VAT na yeye anacheza na TRA halipi asilimia 18 ya kodi hiyo. Alikuwa anaingiza kati ya shilingi milioni saba mpaka nane kwa dakika. Serikali ilipoteza matrilioni ya fedha. Huyu mtu yupo kwenye mikono salama kwa sasa”.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Auawa kwa Fimbo

    By: Unknown On: 22:12
  • Share The Gag
  • ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikosi cha 212 kilichopo Milambo mkoani Tabora, ameuawa kwa kipigo kutoka kwa wafugaji akiwa eneo lake la ujenzi.

    Aliyeuawa katika tukio hilo la juzi katika kijiji cha Usule kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora ni Crius Mkumozi mwenye umri wa miaka 35.

    Mtuhumiwa wa mauaji hayo inadaiwa alikuwa akichunga mifugo kwenye eneo la askari huyo.

    Akizungumza ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Hamisi Issa alisema askari huyo alipigwa fimbo kichwani na begani baada ya kujaribu kuondoa ng’ombe waliokuwa kwenye eneo lake.

    Kamanda alisema mtuhumiwa ambaye hakutaka kutaja jina lake, anashikiliwa kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog

    Serikali Yamtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Achukue Hatua Stahiki Dhidi ya Aliyemtukana Rais Magufuli

    By: Unknown On: 21:29
  • Share The Gag
  • SERIKALI imemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuchukua hatua stahiki katika shauri la kesi ya jinai namba 100 ya Jamhuri dhidi ya Isaac Emily aliyeadhibiwa kulipa faini kwa kumtukana Rais John Magufuli mtandaoni.

    Hayo yamesemwa jana bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe wakati akitoa kauli ya serikali baada ya mwongozo ulioombwa na wabunge wa CCM, Juma Nkamia wa Jimbo la Chemba na Livingstone Lusinde wa Mtera, baada ya hukumu hiyo kutolewa hivi karibuni. Hata hivyo, hatua stahiki hizo hazikuelezwa.

    Alisema nia ya maagizo hayo kwa DPP ni kulinda dhana na dhamira ya adhabu katika mfumo wa haki jinai ambayo hutaka mhukumiwa kujutia kosa lake na wengine kujifunza kutoka kwake.

    Katika maelezo yake, Waziri Mwakyembe alisema kwa hali ilivyo katika shauri hilo, dhana na dhamira ya adhabu haikuweza kufikiwa kwa mwenendo wa kuingiza siasa katika utekelezaji wa hukumu.

    Alisema serikali imejiridhisha na kilichotokea katika shauri hilo na kauli za wabunge walioomba mwongozo kwamba masharti ya adhabu yalikuwa mepesi mno usiolingana na shauri lenyewe.

    Alisema aliyehukumiwa analifanyia siasa suala hilo na kuigeuza adhabu rafiki aliyopewa kuwa burudani ya kisiasa katika mitandao ya kijamii.

    “Mheshimiwa spika, nimejiridhisha na kilichotokea. Madhara ya mwelekeo huu mpya katika haki jinai, ni kuchochea vitendo zaidi vya ukaidi kwa mamlaka za nchi na hivyo kujenga msingi wa vurugu. Hili halikubaliki katika utawala wa sheria. Mdharau mwiba mguu huota tende,” alisema..

    Alisema kosa kama hilo lilitokea Kenya mwaka jana ambapo mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini humo, Alan Okengo (25) alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na kulipa faini ya dola 2,000 (Sh milioni 3.2) kwa kumtukana rais wa nchi hiyo kwenye mitandao ya kijamii.

    Alisema pamoja na umri wake na uwezo wake mdogo wa kulipa faini, adhabu ilibaki palepale ili mkosaji ajutie kosa lake asije akarudia na jamii ijisikie salama.

    Alisema pamoja na kutokuingilia mhimili wa mahakama na taratibu zake kitendo cha kuwapo kwa adhabu ambayo haijutiwi inakiuka dhana na dhamira ya adhabu.

    Alisema kwa shauri la Emily, pamoja na kutiwa hatiani wakili wake aliomba mtuhumiwa alipe faini kwa kuwa hakusumbua mahakama na pia ni kosa lake la kwanza na ana familia.

    Alisema wakati hakimu anamuuliza wakili wa serikali aliiachia mahakama kutoa maamuzi ambayo ilimpatia wakili wa utetezi maombi yake.

    Mwakyembe alisema pamoja na maagizo ya serikali kwa DPP amewakumbusha waendesha mashitaka nchini kuwa macho na waweke mbele weledi na maslahi mapana ya taifa na kamwe wasiyumbishwe na mihemko ya kisiasa katika jamii.
     
    Credit; Mpekuzi Blog