Wednesday, 25 May 2016

Hukumu kesi ya shambulio la Al-Shabab Uganda

By: Unknown On: 23:28
  • Share The Gag
  • Baadhi ya washtakiwa walidai kuteswa wakiwa korokoroni
    Mahakama mjini Kampala leo inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ambapo wanaume 13 wameshtakiwa kuhusiana na mashambulio ya mabomu yaliyotekelezwa na al-Shabaab mwaka 2010.
    Watu zaidi ya 70 walifariki kwenye mashambulio hayo yaliyotekelezwa watu wakitazama fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 2010.
    Kesi hiyo imechukua miaka sita.
    Baadhi ya washtakiwa walikuwa wameambia mahakama kwamba waliteswa na maafisa wa ujasusi wa kanda, Marekani na Uingereza.
    Lakini mahakama ya kikatiba nchini Uganda ilifutilia mbali madai hayo.

    Washtakiwa 13

    Washukiwa ni 13 kutoka Uganda, Kenya na Tanzania. Saba ni Waganda, 5 Waenya na mmoja anatoka Tanzania.
    Wao ni: Bw Habib Suleiman Njoroge, Isa Ahmed Luyima Abubaker Betamatory na Dkt Ismail Kalule.
    Wengine ni Suleiman Hijar Nyamandondo, Hassan Haruna Luyima, Hussein Hassan Agade, Bw Idris Magondu, Mohamed hamid Suleiman na Yahya Suleiman Mbuthia.

    Kutokea kwa shambulio

    Shambulio lilifanyika 11 Julai, 2010 na vituo viwili vilishambuliwa Ethiopian Village Restaurant, Kabalagala na Kyadondo Rugby Club, Nakawa watu waliopokuwa wamekusanyika kutazama fainali ya Kombe la Dunia iliyokuwa ikichezewa Afrika Kusini.

    Idadi ya wahanga

    Watu 74 walifariki katika shambulio hilo na wengine 70 kujeruhiwa. Takriban watu 60 waliouawa ni wa kutoka Uganda. Wengine waliofariki dunia ni kutoka mataifa ya Ethiopia, Eritrea, India na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na mmoja kutoka Ireland na Marekani.

    Kuendeshwa kwa kesi

    Kesi ilianza miaka mitano baadaye baada ya kucheleweshwa na hatua ya washukiwa kupinga kupelekwa kwao nchini Uganda na kudai kuteswa na vikosi vya usalama.
    Lakini Oktoba 2014 mahakama ya kikatiba ilitupilia mbali kesi yao na hivyo kesi kuanza.
    Wanashtakiwa makosa ya: ugaidi, mauaji na kuwa wanachama wa kundi la kigaidi.
    Jaji wa mahakama kuu aliyesikiliza kesi hiyo ni jaji Alfonso Owiny Dollo.

    Mwendesha mashtaka kuuawa

    Wakati mmoja muongoza mashtaka aliuawa na watu wasiojulikana waliokuwa na bunduki.

    Chanzo BBC.


    Suala la ujangili latikisa Bunge

    By: Unknown On: 23:26
  • Share The Gag

  • Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe.

    MBUNGE wa Viti Maalumu, Catherine Magige (CCM) amesema Bunge linapaswa kufahamu ni mbunge gani ambaye anajihusisha na ujangili, kwani hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria.
    Magige, ambaye amependekeza sheria ibadilishwe majangili ama wapigwe risasi au wafungwe jela maisha, ni miongoni mwa wabunge ambao walivalia njuga suala la ujangili jana wakati wakichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

    Kwa upande wake, serikali kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17, alisema majangili nguli wanane wenye mitandao ya kimataifa ni miongoni mwa wahalifu 53 waliohukumiwa baada ya kukutwa na hatia.
    Wabunge majangili? Akichangia, mbunge Magige alisema inasemekana baadhi ya wabunge wanajihusisha na ujangili hivyo akashauri ni vyema wakafahamika. “Inasemekana baadhi ya wabunge wanajihusisha na ujangili. Huyo jangili ni nani? Munde Tambwe, Catherine Magige au Ally Keissy,” alihoji mbunge huyo wa Viti Maalumu kutoka Mkoa wa Arusha. “Hakuna aliye juu ya sheria, tunaambiwa majangili tunao humu ndani, tunataka tuwafahamu, tusinyooshee vidole wengine,” aliongeza Magige.

    Alisema ujangili umekithiri nchini na tembo wanatoweka. Alipendekeza sheria ibadilishwe majangili ama wapigwe risasi au wafungwe jela maisha. Majangili nguli watajwa Profesa Maghembe alisema katika mwaka 2015/16, doria zilifanyika ndani na nje ya Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu kwa siku-doria 109,474 na ziliwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 1,176 na kesi 654 zilifunguliwa.
    “Kesi 161 zilimalizika kwa wahalifu 53 kuhukumiwa kifungo cha jumla ya miezi 6360 na shilingi 363,904,800 kulipwa kama faini. Kati ya wahalifu waliohukumiwa, wanane ni majangili nguli wenye mtandao wa kimataifa,” alisema waziri. Alisema katika doria zilizofanyika, nyara mbalimbali za serikali zilikamatwa, ambazo ni pamoja na wanyamapori hai; mijusi 315, kobe 202, tumbili 81 na nyani mmoja.
    Nyara nyingine ni vipande 253 vya meno ghafi ya tembo vyenye uzito wa kilo 634 na vipande 34 vya meno ya tembo yaliyochakatwa vyenye uzito wa kilo mbili. “Vilevile, kilo 10,096 za nyamapori wa aina mbalimbali na ngozi 39 za wanyamapori zilikamatwa.

    Aidha, bunduki 85 na risasi 1,235 za aina tofauti zilikamatwa,” alisema Maghembe. Katika kudhibiti ujangili wa wanyamapori, wizara kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi ilibaini kuwa ujangili unafanyika katika ngazi tano.
    Alitaja ngazi hizo kuwa ni baadhi ya wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayopakana na hifadhi na watumishi wasio waaminifu. “Wawindaji haramu wanaojihusisha moja kwa moja na kuua wanyama, wasafirishaji na madalali, wawezeshaji kwenye ngazi ya nchi wanaonunua nyara, kusambaza vitendea kazi (silaha) ambao ni kiungo kati ya majangili nguli na watakatishaji fedha na wahalifu walioainishwa katika ngazi tatu za awali na majangili nguli wa kimataifa,” alisema.

    Alishukuru mamlaka zinazosaidiana nazo katika vita dhidi ya ujangili ambavyo ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Kikosi cha Kuzuia Makosa Makubwa na mhimili wa Mahakama. Wahoji aliyetoa leseni Wakati huo huo, katika uchangiaji, wabunge wamekuja juu na kuibana serikali wakitaka kufahamu ni nani aliyeipa tena leseni Kampuni ya Green Miles Safaris Limited baada ya kufutiwa kwa kujihusisha na uwindaji haramu.

    Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko (CCM) alihoji ni nani aliyeipa tena leseni Kampuni ya Green Miles Safaris Limited kwa sababu leseni yao ilishafutwa. “Hili la Green Miles Safaris Limited nalijua…ilikiuka taratibu za uwindaji wa wanyamapori na ilikuwa disqualified.
    “Ilinyang’anywa leseni, nilikuwa kwenye Tume…wataalamu wa wizara watoe maelezo,” alisema mbunge huyo wa Kasulu. Katika maoni yao, Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge pia ilihoji suala hilo ikisema kampuni hiyo ya uwindaji ilinyang’anywa leseni kutokana na uwindaji usiozingatia sheria na taratibu.

    “Kambi Rasmi ya Upinzani inashangaa ni kwa nini mheshimiwa waziri wa sasa kwa barua yake ya Mei 9, 2016 inaonekana kuwa inaipatia tena kampuni hiyo kitalu cha uwindaji wakati tayari ilikwisha pokonywa leseni kwa kuwa ilivunja sheria,” alisema Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Esther Matiko.
    Katika mchango wake mwingine, Nsanzugwanko alipendekeza serikali kuwaondoa kwa ustaarabu mifugo inayoingia katika maeneo ya hifadhi. Aidha, alishauri kuwa serikali iyagawe maeneo yasiyo na tija ya hifadhi ambayo yako kwa muda mrefu na hayatumiki kwa kuyahuisha na kuwapa wananchi ili wafanye shughuli za maendeleo.

    Mbunge wa Bukombe, Dotto Biteko (CCM), alikataa kuunga mkono hoja hiyo akisema wananchi wake wanauawa na mifugo inauawa katika mapori ya akiba ya Muyowosi na Kigosi. Biteko alisema ng’ombe 125 na punda wameuawa na ng’ombe 603 wametaifishwa na kuna unyanyasaji mkubwa wa wananchi wanaooingia katika hifadhi. Alisema ziko nyumba 40 ziko katika vijiji ambavyo vimeandikishwa kisheria, hivyo wana haki zote kisheria, lakini wananyanyaswa na askari wa wanyamapori.
    Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF) pia alalamikia unyanyasaji wa askari wa wanyamapori akisema kuna vijiji 21 vimeandikishwa katika jimbo lake, lakini watu wake wanaoishi kwa hofu kubwa. Kwa upande wake, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) alisema Bunge linapaswa kujisafisha kuhusu tuhuma za kuwa kuna mbunge ni jangili.

    Msigwa alisema tuhuma hizo ni kashfa kwa Bunge kwa sababu suala hilo limekuja huku chombo hicho cha kutunga sheria kikiwa kimewahi kutuhumiwa kuwa kuna wala rushwa na walevi. “Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesikia hapa mbunge mmoja amesema asubuhi kuwa kuna mbunge ni jangili. Magazeti yameonesha kuwa gari zake zimetumika katika ujangili.
    Bunge lazima lisafishwe katika hili, maana Bunge hili limewahi kutuhumiwa kwa rushwa na kuwa wengine ni wanapiga mtindi,” alisema Msigwa. Alisema ni lazima Bunge lijisafishe kwa tuhuma hizo, kwani pia mbunge anayetuhumiwa kwa kuwa jangili, anatajwa kuvamia eneo la hifadhi yawanyamapori wilayani Meatu. Alisema si sahihi kwa mtu kuchimba madini ndani ya hifadhi,hivyo anataka kufahamu mbunge huyo amepewaje eneo la kuchimba madini humo.

    Aidha, Msigwa alizungumzia suala la Kampuni ya Green MilesSafaris Limited, akihoji kuwa kampuni hiyo ilipokonywa leseni za uwindaji kwa kukiuka taratibu, nani amewapa tena leseni hiyo. “Kampuni hii haina sifa kwa sababu imekiuka uhifadhi,haikupewa vitalu, haina sifa, imefanya infringement zaidi ya 11, hawana sifa za uwindaji.
    Tujue nani Operesheni Tokomeza Alitaka ripoti ya Tume Maalumu ya Kimahakama iliyoundwa kufanya tathmini ya Operesheni Tokomeza kuwekwa hadharani na kumtaka Spika aombe kwa serikali ili iwekwe hadharani.

    Hoja hiyo iliungwa mkono na Kambi ya Upinzani ikisema ni wakati mwafaka sasa kuelewa ni majangili wangapi kuelezwa baada ya operesheni hiyo kumalizika mali zao zimekamatwa na tayari kesi zao ziko mahakamani na wangapi wamefungwa.
    Katika maoni yao, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii ilisisitiza serikali kuweka utaratibu wa kuwalipa fidia au kifuta machozi kwa wananchi walioathiriwa na operesheni hiyo.
    Kuhusu ujangili, Kamati ilishauri kuwa kesi za ujangili zisikilizwe kwa haraka na adhabu kali zinatolewa kwa watakaokutwa na hatia. Aidha, ilishauri serikali kuchukua hatua za haraka kwa kuwashirikisha wananchi kutatua migogoro ya mipaka kati ya maeneo yanayohifadhiwa na wananchi wanaoishi kuzunguka maeneo hayo.

    Chanzo HabariLeo.

    Kenya yawasaka wasukiwa wa Islamic State

    By: Unknown On: 23:21
  • Share The Gag
  • Mkuu wa polisi amesema washukiwa wawili wamekamatwa
    Polisi nchini Kenya inaendelea na msako wa kuutia mbaroni mtandao wa kundi la wapiganaji linalojiita Islamic State ambalo linataka kukita mizizi yake nchini Kenya kwa lengo la kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wananchi wasio kuwa na hatia. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na inspekta mkuu wa polisi.
    Kauli hiyo imetolewa baada ya polisi nchini Kenya kuwatia mbaroni watu wawili wanaoshukiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la wapiganaji la IS.
    Kwa mujibu wa polisi, kukamatwa kwa wawili hao ambao ni Mwangolo Mgutu na Abubakar Jillo Mohammed kumezuia mashambulizi ya kigaidi yaliyokuwa yakipangwa kwa kutumia vilipuzi na silaha nyingine katika mji wa Nairobi na Mombasa.
    Mbali na kukamatwa kwa washukiwa hao wawili, polisi pia imepata vitu mbalimbali katika nyumba ya Kiguzo Mwangolo kama vile misumari, betri, waya na mbolea ambazo inadaiwa zingetumika kutungezea bomu la nyumbani.
    Polisi imeendelea kusema, katika uchunguzi wake wa mwanzo, imebaini kuwa Kiguzo na Abubakar ni miongoni mwa waandishi wa makala iliyokuwa inasambaa kupitia mtandao ambao ilikuwa ikielezea kuwepo kwa kundi la Jahba katika eneo la Afrika Mashariki ambalo limetangaza kumuunga mkono kiongozi wa ISIS Abubakr Al-Baghdadi.

    Chanzo BBC.

    Lowassa Ajisafisha Tuhuma za Kukwapua ardhi Ya Wananchi na Kujimilikisha

    By: Unknown On: 23:20
  • Share The Gag

  • Siku chache  baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kulieleza Bunge kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alijimilikisha shamba la Makuyuni Wilayani Monduli mkoani Arusha, Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga amejitokeza kutoa ufafanuzi unaomsafisha.

    Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Kalanga alisema kuwa Lowassa hamiliki shamba hilo la Makuyuni kwakuwa tangu Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alipofuta hati ya umiliki wa shamba hilo kutoka kwa raia wa Kigeni aliyemtaja kwa jina la Stein, bado halijamilikishwa rasmi kwa wananchi na ndio ilikuwa hoja yake.

    Alisema kuwa maelezo ya Lukuvi hayakuwa na ukweli  na kwamba alichanganya kati ya shamba hilo la Mkuyuni na shamba la Manyara Ranchi ambalo hati yake ilifutwa tangu mwaka 2000 na kukagawiwa kwa wananchi wa Monduli ambapo Lowassa alisaini hati miliki yake kama muwakilishi wa wananchi wa Wilaya hiyo kwakuwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini ya Ardhi (Tanzania Land Trustee (TLCT).

    “Jambo la kushangaza ni pale Waziri alipochanganya shamba hilo na lile la Manyara Ranchi ambalo hati yake ilifutwa tangu mwaka 2000 na kugawiwa kwa wananchi. Hati miliki ya shamba hilo la Manyara Ranchi ilisainiwa na Lowassa ambaye wakati huo alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Land Trustee(TLCT),” alisema

    Awali, Waziri Lukuvi alieleza kuwa Shamba hilo la Mkuyuni linapaswa kumilikishwa kwa wananchi lakini nyaraka zinaonesha kuwa hati yake imesainiwa na Lowassa na kwamba Serikali itamnyang’anya na kulirejesha kwa wananchi.

    Juzi, Lowassa aliahidi kuwasiliana na Mbunge huyo ili kufuatilia kauli aliyoitoa Waziri Lukuvi dhidi yake kuhusu kujimilikisha shamba hilo ili aweze kutoa ufafanuzi kwani hakuna ardhi anayoimiliki kinyume cha taratibu.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog

    Tuesday, 24 May 2016

    Mkenya Afunga Ndoa na Mwanaume Mwenzake

    By: Unknown On: 02:03
  • Share The Gag

  • KATIKA matukio ambayo wanaume wa Kenya wanaoana na wanaume wenzao katika nchi zinazoruhusu jambo hilo, mwanamme mmoja wa Nakuru, Kenya, amefunga ndoa na profesa wa hisabati wa Marekani.

    Bw.  Ben Gitau (33) na Bw. Steve Damelin walioana wiki iliyopita huko Ann Arbor, Michigan, Marekani, Jumamosi alasiri ambapo baada ya tukio hilo wawili hao walionekana wakibusiana na kukumbatiana ambapo marafiki na wanafamilia walipiga vigelegele na kushangilia.

    Hata hivyo, mshauri mmoja wa masuala ya kifamilia , Mchungaji Philip Kitoto wa International Christian Centre, Nairobi,alilaani ndoa hiyo akisema: “Kiutamaduni na kwa mujibu wa Bibilia,  ndoa na kujamiiana kati ya watu wa jinsia moja ni dhambi.”

    “Biblia iko wazi kwamba Mungu alituumba kwa taswira yake; mme na mke.  Katika kitabu cha Mambo ya Walawi 18:22 Mungu anamwonya  mwanaume kutofanya ngono na mwanaume  mwenzake  kama anavyofanya na mwanamke.”

    Bw.  Kararu Ririe, rafiki wa karibu wa wanandoa huyo ambaye ni Mkenya aliyewahi kukiri kwamba ni shoga anayeishi California, Marekani, alitume ujumbe kwenye mtandao wa twitter baada ya ndoa hiyo akiandika kwamba: “Jioni hii nilimpongeza rafiki yangu, Ben na mumewe Steve, kwa ndoa yao.  Ni jambo adimu kwa Mkenya kuwa jasiri kiasi hicho.  Hongera.”

    Gitau alikuwa anaishi Atlanta, Georgia, kabla ya kuhamia California.  Kwa mujibu wa mwanafamilia  mmoja aliyezungumza na gazeti la Daily Nation, Gitau alikutana na mchumba wake huko Atlanta ambako Damelin alikuwa mwanafunzi wa shahada ya uzamivu (PhD) katika Chuo cha Teknolojia cha Georgia.

    Katika kulaani tukio hilo, Mchungaji  Kitoto alisisitiza kwamba tendo la ndoa kati ya mwanamme na mwanamke liliwekwa kwa ajili ya uzazi.

    Ndoa za jinsia moja zilihalalishwa katika Jimbo la Michigan mwaka jana mwezi Julai na Mahakama Kuu ya Marekani iliyoondoa sheria zinazopinga ndoa za watu wa jinsia moja mradi tu wawe wanapendana.

    Source: Daily Nation

    Credit; UDAKU SPECIAL

    Maalim Seif Sharif Hamad Aitwa Polisi Kuhojiwa

    By: Unknown On: 01:59
  • Share The Gag
  • Jeshi la Polisi Zanzibar litamhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad Ijumaa ya wiki hii kuhusu masuala mbalimbali ambayo hata hivyo, hayakuwekwa wazi.

    Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Makame alisema jana: “Natambua kuwa wasaidizi wangu watazungumza naye Ijumaa. Wao ndiyo wanajua watamhoji nini.”

    Alipoulizwa kuhusu mahojiano hayo, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi naye hakuweka wazi badala yake alisema kuna masuala mengi ambayo ofisi yake inahitaji kuyafahamu kutoka kwa Maalim Seif.

    Hii ni mara ya kwanza kwa Maalim Seif kuhojiwa na polisi tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu ambao kwa Zanzibar ulirejewa Machi 20, baada ya ule wa Oktoba 25 mwaka jana kufutwa.

    Maalim Seif ambaye kabla ya uchaguzi huo alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alipinga kurudiwa kwa uchaguzi huo msimamo ambao pia ulichukuliwa na chama chake.

    Kiongozi huyo amekuwa akitoa matamko kadhaa ya kuwashawishi wananchi kupinga utawala wa Serikali iliyopo madarakani.

    Akiwahutubia wafuasi wake huko Pemba hivi karibuni, Maalim Seif alisema Serikali ya CCM imeanza kutikisika kutokana na vikwazo vinavyoendelea kuwekwa na wahisani pamoja na hatua ya chama chake CUF kutowatambua viongozi wake pamoja na Serikali. 
    “CCM wajue wamekalia kuti kavu, siku yoyote wataanguka... tufanye kazi mpaka haki yetu tuhakikishe imerudi na wenzetu hawana safari ya kudumu,” alisema.

    Aliwataka wanachama wake kuonyesha kwa vitendo kutoitambua Serikali ikiwamo kukataa kulipishwa kodi za ovyovyo pamoja na kujitenga na viongozi wa Serikali katika utekelezaji wa majukumu yao.

    “Mfano tunaweza kuamua siku fulani kuanzia saa sita, tunasimamisha vyombo vyote vya usafiri na siku nyingine tunaamua kupiga honi Zanzibar nzima kuonyesha hatuitaki Serikali ya CCM,” alisema huku akishangiliwa na umati uliofurika katika ofisi za chama hicho.

    Mapema jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo alisema kuwa amesikia juu ya wito huo lakini hakuwa amepata taarifa rasmi kutoka kwa mkuu wake.

    “Nimesikia kama mlivyosikia ninyi,” alisema na kuongeza: “Nimeelezwa pia hata leo Kamishna wa Polisi Zanzibar alikuwa na mahojiano naye.”

    Kuhusu hilo Kamishna Makame alisema: “Sijaonana wala kuzungumza naye leo. Hiyo si kweli.”

    Juzi, wakati akizindua ripoti ya Uvunjifu wa Haki za Binadamu uliofanyika visiwani humo kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema wanazo taarifa za Serikali kutaka kuwakamata viongozi waandamizi wa chama hicho na kuwashikilia.
    Alisema wamebaini mpango wa kukamatwa kwao na kuwekwa kwenye Mahakama za bara ili kuwanyamazisha Wazanzibari.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog

    Wanasayansi China watumia nguruwe kutibu upofu

    By: Unknown On: 01:55
  • Share The Gag
  • Konea kutokwa kwa nguruwe hutibiwa na kutolewa DNA kabla ya kupandikizwa
    Wanasayansi wa Uchina wamefaulu katika tiba yao mpya ya majaribio ya kutibu upofu.
    Walitumia nguruwe katika majaribio hayo ya tiba ya kuondoa upofu, ambapo walitumia konea kutoka kwa wanyama hao.
    Sasa wamesema wana imani kwamba hilo litafaa sana kutokana na uhaba wa konea za binadamu.
    Inakisiwa kuwa Wachina wapatao 5 milioni wanakabiliwa na matatizo ya konea, sehemu ya mbele ya jicho iliyo ngumu na inayowezesha miali ya mwanga kupenya.
    Lakini ni konea 5,000 pekee ambazo hupatikana kila mwaka.
    Matatizo ya konea husababisha watu wengi kuwa kipofu.
    Njia hiyo mpya ya kutibu upofu imeanza kutumiwa baada ya kuidhinishwa na serikali mwaka jana.
    Konea kutoka kwa nguruwe hutibiwa na kutolewa bakteria na virusi, pamoja na kutolewa DNA ya nguruwe, kabla ya kupandikizwa katika jicho la mwanadamu.
    Wakosoaji wa mpango huo wanasema Uchina inaenda kwa kasi sana, bila kuangazia madhara ya mpango huo kwa kipindi kirefu.

    Chanzo BBC.