Tuesday, 24 November 2015

Majibu ya Ikulu kuhusu CT Scan na MRI, Wizi wa dawa za Serikali, Huduma Mbaya Kwa Wagonjwa na Safari za Nje Kwa Viongozi

By: Unknown On: 01:57
  • Share The Gag
  • Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue jana alifanya ziara katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni muendelezo baada ya Rais Dk. MAGUFULI kufanya ziara ya kushtukiza.

    Baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukagua vitanda vilivyonunuliwa baada ya agizo lake, Sefue alitoa maamuzi yaliyofikiwa…
     
    Majibu kutoka Ikulu kuhusu mashine za CT Scan na MRINimekagua mashine hizi za kukagua magonjwa MRI na CT Scan, chanzo cha kuharibika tena ni kukaa muda mrefu bila kutumika,sasa hivi spea zote zimefika, kazi ya kutengeneza inaendelea, MRI nimehakikishiwa ndani ya siku tatu itakuwa inafanya kazi, kuhusu CT Scan nimeambia kesho(leo) inaweza kuanza kufanya kazi”..
     
    “Lazima mafundi kutoka Philips  wakae muda wa wiki moja baada ya kutengenezwa kujiridhisha zimekamilika..bado tuna mpango wa kuongeza mashine hizi ili angalau tume na mbili mbili..,kuhusu madeni ya mshine hizo..
     
    "Ni kweli kulikuwa na madeni lakini tumeanza kuyalipa kwa sasa suala hilo halipo tena, tulikuwa tunadaiwa na Philips bilioni 7 na Serikali tayari ililipa bilioni 3 nyingine zinapaswa kulipwa na waliokuwa wakipata huduma ya mashine hizo“… Ombeni Sefue.

    Maduka ya Bohari ya dawa MSD kujengwa ndani ya hospitali kubwa..“Tuna tatizo la kibajeti, tunahitaji bajeti ya kama bilioni 248, bajeti unakuta inafikia kama bilioni 70, hili inabidi tushughulike nazo hasa katika hospitali kubwa pamoja na zile za rufaa, MSD wanapaswa kufungua maduka yao ndani ya hospitali..na lazima kuwa na dawa zote, hospitali ya Muhimbili duka la madawa litafunguliwa rasmi Jumatatu”..Ombeni Sefue.
     
    Ishu ya wizi wa dawa za Serikali pia imesikika...“Tutumie mifumo ya TEHAMA kuhakikisha hakuna dawa ya Serikali inaibiwa, pia tujue kwamba kila dawa inatumiwaje na daktari, ufumbuzi wa matatizo haya upo, kwa wale wa maduka ya dawa binafasi ambao wanajijua wanatumia dawa za serikali michezo hiyo, basi, dawa zetu tutakuwa tunaziwekea nembo, ukigundulika ujue mwisho wako basi, mnapaswa kutambua dawa hizi zinanunuliwa na kodi ya wananchi hivyo tutadhibiti tabia hii” ...Ombeni Sefue.
     
    Huduma mbaya kwa wagonjwa “Tutoe huduma nzuri kwa wananchi, tuwahudumie kwa upendo na wakati,  kuanzia sasa kila mtumishi wa umma lazima avae jina lake ili anayemuhdumia ajue anahudumiwa na nani, nitaanza na mimi..ili ikitokea malalamiko ajue anaanzia wapi, na lazima kila ofisi iwe na dawati la msaada ili kila mwananchi aweze kupiga simu na kuweza kutatuliwa tatizo lake”Ombeni Sefue.
     
    Kuhusu safari za nje kwa viongozi...“Tumetumia fedha nyingi sana kwenda nje, nyingine za lazima na nyingine sio za lazima, mfano mafunzo sasa ni mwisho, tunavyo vyuo vingi vyenye uwezo wa kutoa mafunzo badala ya kwenda nje ama ni rahisi kuleta mtaalam hapa kuliko kupeleka watu 10 kwenda kwenye mafunzo..
     
    "Sasa hivi itakua mbinde mtu kuweza kusafiri..si kwamba hatutahudhuria mikutano lakini Rais amesema mabalozi wetu watatumika pale inapobidi”...Ombeni Sefue.
    Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa Mashine ya CT-Scan katika hospitali hiyo. 23 Novemba, 2015
    Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (mwenye suti ya kijivu), akimsikiliza mmoja wa Wagonjwa aliyelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), ambayo ilipata vifaa mbalimbali kutokana na agizo la Mhe. Rais la kuboresha huduma katika Taasisi hiyo. 23 Novemba, 2015
    Pichani; Mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo inafanyiwa matengenezo. 23 Novemba, 2015
     Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (wa tatu kulia), akitoa maelezo kuhusiana na ziara yake hiyo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari. 23 Novemba, 2015
    Credit; Mpekuzi blog

    Uturuki yadungua ndege mpaka wake na Syria

    By: Unknown On: 01:55
  • Share The Gag
  • Runinga ya taifa imeonyesha ukanda wa video ulioonyesha ndege ikianguka
    Ndege za kijeshi za Uturuki zinaripotiwa kudungua ndege ya kijeshi isiyojulikana karibu na mpaka wake na Syria.
    Afisa wa jeshi la Uturuki ameambia shirika la habari la Reuters kwamba ndege za kijeshi za Uturuki aina ya F-16 zilishambulia ndege hiyo baada ya kuionya kwamba ilikuwa imeingia anga ya Uturuki bila idhini.
    Runinga ya taifa ya Uturuki imepeperusha ukanda wa video unaoonyesha ndege ikianguka milimani karibu na mpaka wake na mkoa wa Hatay.
    Ndege za kijeshi za Syria na urusi zimekuwa zikishambulia wapiganaji wa Kiislamu pamoja na waasi wanaoungwa mkono na mataifa ya Magharibi eneo hilo.

    created by BBC Swahili.

    Kenya yatangaza sikukuu kwa sababu ya Papa

    By: Unknown On: 01:51
  • Share The Gag
  • Serikali ya Kenya imetangaza kuwa Alhamisi Novemba 26 itakuwa siku ya mapumziko ambayo pia itatumiwa kama siku ya kitaifa ya maombi ya kujitafakari.
    Siku hiyo itakuwa ya pili kwa Papa Francis kuwa nchini Kenya baada ya kuwasili Novemba 25.
    Msemaji wa ikulu Manoah Esipisu amesema kupitia taarifa kwamba: “Kwa kuwa tuna heshima kubwa ya kuwa mwenyeji wa Papa wakati huo, atatuongoza kwa mada ya siku hiyo”.
    Papa Francis, ambaye atakuwa kwenye ziara yake ya kwanza kabisa Afrika anatarajiwa kuondoka Kenya kuelekea Uganda Ijumaa Novemba 27.
     
    Created by BBC Swahili.

    Marekani yatoa tahadhari kwa raia wake

    By: Unknown On: 01:48
  • Share The Gag
  • Serikali ya Marekani imetoa tahadhari ya kusafiri duniani kote kwa raia wake, ikiwaonya kuwepo kwa ongezeko la tishio la kigaidi.
    Tahadhari hiyo inasema taarifa zilizopo hivi sasa zinaashiria kwamba makundi kama vile Islamic State, al-Qaeda na Boko Haram wanaendelea kupanga mashambulio katika maeneo tofauti.
    Inawataka wasafiri kuwa makini hasa wanapokuwa katika mikusanyiko ya watu au pindi wanapotumia usafiri wa umma.
    Hata hivyo, afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameiambia bbc kwamba hakuna sababu ya kuamini kwamba raia wa Marekani ndio walengwa.
    Mamilioni ya raia wa marekani watasafiri wiki hii kwa ajili ya sikukuu ya kutoa shukrani siku ya alhamisi.
    Created by BBC Swahili.

    Magufuli Atikisa Mitandao Ya Kijamii Nchi Kenya.......Wakenya Wamwagia Sifa Kibao, Watamani Awe Rais Wao

    By: Unknown On: 01:44
  • Share The Gag
  • Uchapakazi wa Rais Dkt John Magufuli unatuma ujumbe si kwa maafisa wa Tanzania pekee, bali na nchi za jirani pia na kuwaacha viongozi wa nchi hizo kwenye wakati mgumu.
     
    Kenya ambayo imekuwa ikifuatilia siasa za Tanzania tangu wakati wa kampeni, imeonesha kupenda mbinu za Magufuli na wananchi wake wanatamani mtu kama yeye.
     
    Kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani, Magufuli amefanya mambo makubwa na wananchi wamependa.
     
    Ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali ya Muhimbili ilifichua uovu mwingi na kupelekea kufutwa kwa bodi ya wakurugenzi wa hospitali hiyo na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk Hussein Kidanto.
     
    Ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za serikali kwaajili ya kugharamia safari za nje za viongozi wa nchi, Magufuli aliamua kuzisitisha mara moja.
     
    Dkt Magufuli pia alielekeza kiasi cha shilingi milioni 225 zilichangwa kwaajili ya kugharamia hafla ya wabunge kupongezana mjini Dodoma zipelekwe kwenda kununua vitanda. Badala yake shilingi milioni 15 pekee zilitumika kwaajili ya sherehe hiyo. 
     
    Siku chache baadaye vitanda hivyo na vifaa vingine vilinunuliwa na kupelekwa Muhimbili.
     
    Jumatatu hii Magufuli alitangaza kuondoa sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru December 9 na fedha za maandalizi hayo zitumike kwa mambo mengine muhimu.
     
    Hayo na mambo mengine yamefanya Dkt Magufuli atrend nchini Kenya.
    Credit; Mpekuzi

    Uhuru hapa ni kazi tu

    By: Unknown On: 01:40
  • Share The Gag

  • Rais Dk John Magufuli.

    RAIS John Magufuli amewataka Watanzania popote walipo kusherehekea siku ya Uhuru, Desemba 9, 2015, kwa kufanya kazi. Taarifa iliyotolewa na Ikulu Dar es Salaam jana, ilisema kwamba maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu (2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi (Uhuru na Kazi) nchini.
    “Mheshimiwa Rais ameelekeza Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo,” ilisema taarifa hiyo.
    Aidha, ilisema kwa kuwa sherehe za Uhuru na Jamhuri huendana na maandalizi mbalimbali ambayo yanatumia fedha, kwa kuzingatia kuwa siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya kazi, fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii, ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali na vitanda vya hospitali kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua.
    “Ieleweke kuwa sherehe za Uhuru na Jamhuri ni muhimu katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu. Hivyo, sherehe hizi zitaendelea kuadhimishwa kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka 2016,” ilifafanua. Maamuzi hayo ya rais yamefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Sikukuu za Kitaifa (The Public Holidays Act, Cap 35) pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko.
    Awali, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliwaeleza waandishi wa habari kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuwa Dk Magufuli amebadilisha mwelekeo wa namna ya kusherehekea miaka 54 ya Uhuru, Desemba 9, mwaka huu, kwa kuwataka Watanzania kuhakikisha siku hiyo wanaitumia kwa kufanya usafi ili kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu. “Ugonjwa wa kipindupindu ni jambo linalomkera Rais Magufuli.
    Amekuwa akisema hivi kweli tunasherehekea miaka 54 ya Uhuru, lakini bado tunashambuliwa na kipindupindu? Ndio maana ameamua kuchukua hatua kwa kuhakikisha nchi nzima wanafanya usafi katika siku hiyo ya kusherehekea Uhuru,” alisema Balozi Sefue. Alisema ugonjwa huo wa kipindupindu chanzo chake kikubwa ni uchafu, hali inayoonesha kuwa bado Tanzania kuna haja kubwa ya kushughulikia uchafu ili kuondokana na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
    Aliwataka wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri na makatibu tawala wote nchini, kuanza kujiandaa na kuweka mikakati ya namna ya kufanya usafi huo katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kuandaa vifaa vya kusafishia mazingira. Hii ni mara ya kwanza kwa sherehe za Uhuru kutosherehekewa kwa gwaride tangu Tanganyika (sasa Tanzania Bara) kupata Uhuru wake Desemba 9, 1961 kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza.
    Aidha, tangu aingie madarakani na hata katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge mjini Dodoma wiki iliyopita, Dk Magufuli ametangaza kubana matumizi ya serikali yake kwa kuchukua hatua kadhaa zikiwamo kufuta ziara za nje ya nchi isipokuwa kwa vibali maalumu, kufuta mikutano isiyo ya lazima katika hoteli kubwa, kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri na sherehe mbalimbali kama ile ya uzinduzi wa Bunge hilo la 11.
    Balozi Sefue alisema kwa mujibu wa Dk Magufuli, hataki kusikia baada ya Desemba, kuna mgonjwa wa kipindupindu sehemu na kwamba endapo kutakuwa na mgonjwa anayesumbuliwa na ugonjwa huo, mkoa husika uongozi wake watawajibika na kujieleza. Aliwataka wakurugenzi wa Halmashauri, kuhakikisha kuwa sheria ndogo za halmashauri zinazotungwa na kupitishwa zinatekelezwa ipasavyo ili kudhibiti matatizo kama hayo ya uchafu uliokithiri unaosababisha milipuko ya magonjwa.
    Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando, alisema ipo Sheria ya Afya ya Jamii mwaka 2003 ambayo inatoa adhabu kwa mtu yeyote atakayekutwa akichafua mazingira ya kifungo cha miezi mitatu au faini ya Sh milioni moja au vyote kwa pamoja. “Ndio maana tunasema sheria zipo, lakini hazifuatwi, sasa huu ni mwanzo tunataka kuhakikisha suala hili la uchafu linadhibitiwa,” alisisitiza.
    Novemba 8, mwaka huu, Dk Mmbando alisema kuwa ugonjwa huo umetapakaa katika mikoa 14 nchini, ukiwakumba watu 7,825 na kuua watu 106. Alisema kati ya watu hao, 3,746 sawa na asilimia 67 wanatoka katika Jiji la Dar es Salaam. Mikoa mingine yenye ugonjwa huo ni Pwani, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mara, Singida, Tanga, Kilimanjaro, Shinyanga, Rukwa, Iringa, Geita na Kigoma. Advera Bulimba

    Created by Gazeti la HabariLeo

    ‘Rekodi sheria mkononi uzawadiwe’

    By: Unknown On: 01:36
  • Share The Gag

  • Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Advera Bulimba.   

    JESHI la Polisi nchini limekemea tabia inayoendelea kujengeka miongoni mwa baadhi ya wananchi ya kutoheshimu sheria na kujichukulia sheria mikononi kwa kuwapiga, kuwadhalilisha watuhumiwa, kuwachoma na kuwaua.
    Aidha imetangaza zawadi kwa mwananchi yeyote atakayerekodi tukio la aina hiyo na kulifikisha kwao. Imeelezwa kuwa kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, watuhumiwa 829 wameuawa na wananchi.
    Polisi imewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kukomesha tabia hiyo na kuahidi kuwa mwananchi yeyote atakayerekodi tukio la watu wanaojichukulia sheria mkononi na kulifikisha polisi kwa siri atapewa zawadi.
    Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Msemaji wa jeshi hilo, Advera Bulimba alisema idadi ya watu hao waliokufa imeongezeka ikilinganishwa na watuhumiwa 785 waliouawa kwa sababu kama hizo kwa kipindi kama hicho mwaka 2014.
    “Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia hiyo ya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuwafanyia vitendo vya kikatili ikiwemo kuwadhalilisha kwa kuwavua nguo watuhumiwa wanaoshukiwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu bila kuwafikisha kwenye vyombo vya dola jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za nchi,” alifafanua msemaji wa Polisi.
    Alisema takwimu zinaonesha wazi kwamba tabia hiyo inaendelea kujengeka na kuonekana kwamba ni jambo la kawaida, lakini ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu na sheria za nchi.
    Bulimba alisema makamanda wote wa polisi nchini wameagizwa kufanya ukamataji wa watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kisingizio cha hasira kali na kuwafikisha mahakamani kwa sababu watu hao kwa mujibu wa sheria, tayari wanakuwa wametenda kosa la jinai.

    Created by Gazeti la HabariLeo.