Monday, 21 August 2017

Madereva Daladala Kituo cha Simu 2000 Wagoma

By: Unknown On: 11:31
  • Share The Gag
  • Baadhi ya madereva wa daladala zinazotumia kituo cha mabasi cha Simu-2000 Mawasiliano kuongezewa ushuru kutoka Sh 500 hadi 1000 wakati wa kutoka ndiyo sababu mojawapo iliyofanya wagome.

    Mbali na hilo, wamesema ubovu wa barabara hiyo ya Mawasiliano ni sababu nyingine kwa madai ya kwamba magari yao yanaharibika kila kukicha.

    Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema walianza mchakato huo tangu saa 11 alfajiri na kwamba wataendeleza hatua hiyo hadi mamlaka husika itakapotoa mwafaka wa sinofahamu.

    Mmoja wa madereva hao Abdulsalum Hamad amesema waliingia katika kituo kama kawaida lakini wakati wanataka kutoka wakaamriwa kulipa Sh 1000 jambo ambalo hawakukubaliana nalo.

    "Baada ya kuamua kugoma kutolipa kiasi hiki walitushirikilia kwa nusu saa ndipo tukachukua uamuzi wa kugoma kabisa na gari itakayoingia hapa kituo haiwezi kutoka kabisa hadi kieleweke,"amesema Hamad

    Kero nyingi ya muda mrefu waliaamua kuiunganisha  katika mgomo huo ni hatua ya wahusika wa kituo hicho cha kuwatoza faini ga Sh 50000 pindi wakatapobainika kunawa nyuso wakiwa msalani kwani hawaruhusiwa kufanya hivyo.

    Hamad aliwataka wahusika wa kituo kuliangalia suala kwa jicho la tatu suala  la tozo ya Sh 1000  kwani huduma zinatolewa na kituo hicho haziendani na tozo hizo na badala yake waiache ya Sh 500.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog

    Uchaguzi Kenya ghali zaidi Afrika

    By: Unknown On: 11:25
  • Share The Gag
  • SIKU 10 tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Kenya, imeelezwa kuwa nchi hiyo ndiyo inayoongoza kwa kufanya uchaguzi ghali zaidi barani Afrika.
    Aidha, kwa duniani imeshika nafasi ya pili, ikitanguliwa na Papua New Guinea inayotajwa kuwa kinara duniani, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari. Wakati Papua NewGuinea ikitajwa kumgharimu kila mpigakura Dola za Marekani 63 (Sh 132,300 za Tanzania), Kenya imetajwa kumgharimu kila raia wake dola 25.4 (Sh 53,340) ili kulipia gharama za kila kura katika mchakato huo wa kidemokrasia.
    Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Kenya, Kamau Thugge katika taarifa yake kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8, mwaka huu, makadirio ya fedha za uchaguzi yalikuwa Shilingi za Kenya bilioni 49.9, sawa na dola za Marekani milioni 499 (Sh trilioni 1.04 za Tanzania). “Ni gharama za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja katika uchaguzi.
    Gharama za moja kwa moja ni Shilingi za Kenya bilioni 33.3 (Dola milioni 333, sawa na Sh za Tanzania bilioni 700). Kwa mujibu wa mchanganuo uliokuwa umetolewa, dola milioni 429 zilitakiwa kwenda Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), huku kiasi kingine kikisambazwa kwa ajili ya mahakama, taasisi za usalama na msajili wa vyama vya siasa.
    Hii ina maana kwamba, kwa dola 25.4 kwa kila mpigakura kati ya Wakenya milioni 19.6 waliojiandikisha, imetia fora kwa kufanya uchaguzi ghali zaidi katika Bara la Afrika. Inaelezwa kuwa, mwaka 2013 Kenya ilitumia Sh bilioni 26 za nchi hiyo, sawa na Dola za Marekani milioni 260 (Sh bilioni 540) kwa ajili ya uchaguzi mkuu uliomweka madarakani kwa mara ya kwanza Uhuru Kenyatta.
    Kiasi hicho ni takribani mara mbili ya uchaguzi wa mwaka huu. Uchaguzi Mkuu wa Kenya mwaka huu pia umevutia idadi kubwa ya wagombea, ambapo kulikuwa na wagombea 16,259 wakiwania nafasi mbalimbali 1,882 huku katika kiti cha urais kilichowaniwa na wagombea wanane, Uhuru Kenyatta (55) alirejea madarakani baada ya kuvuna asilimia 54 ya kura milioni 15.6 zilizopigwa, akimbwaga kwa mara nyingine mshindani wake, Raila Odinga aliyepata asilimia 44.4 ya kura zote.
    Hata hivyo, Raila aliyewania urais kwa tiketi ya Muungano wa Vyama vya Upinzani (NASA), ikiwa ni mara yake ya nne kuisaka Ikulu ya Kenya, lakini bila mafanikio, amegomea matokeo ya uchaguzi huo akidai haukuwa huru na wa haki, licha ya waangalizi wa kimataifa kuusifia uchaguzi huo kuwa haukuwa na dosari. Raila mwenye umri wa miaka 72, amekwenda mahakamani kupinga rasmi matokeo ya uchaguzi huo.
    Katika Afrika Mashariki, Rwanda ambayo pia imefanya uchaguzi wake mkuu mapema mwezi huu uliomrejesha Rais Paul Kagame madarakani, hivyo kuendelea kuongoza kwa muhula wa tatu, imeelezwa gharama zake za uchaguzi kuwa zimemgharimu kila mpigakura Dola ya Marekani 1.05 (sawa na Sh 2,205 za Tanzania). Ilikuwa na wapigakura waliojiandikisha milioni 6.8.
    Katika mwaka 2010, inakadiriwa kila mpigakura wa Rwanda aliigharimu nchi yake dola 1.71 (Sawa za Shilingi za Tanzania 3,591). Gharama za Uchaguzi Mkuu wa Uganda wa mwaka jana, 2016 zinaonesha zilikuwa sawa na Dola 4 za Marekani (Shilingi za Tanzania 8,400), wakati Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2015 uliomweka madarakani Rais mchapakazi na `kioo’ cha nchi nyingi, Dk John Magufuli ulimgharimu kila mpigakura dola 5.16 (Shilingi za Tanzania 10,836).
    Uchaguzi wa Ghana wa mwaka jana umetajwa ndiyo uliokuwa na gharama za chini zaidi barani Afrika, kwa wastani wa dola 0.70 (Sh 1,050 za Tanzania), wakati kiwango cha chini duniani ni wastani wa dola 5 (Sh 10,500 za Tanzania). Nigeria, taifa lenye watu milioni 186 ambalo lina wapigakura takribani milioni 70, mwaka 2015 lilitajwa kutumia dola milioni 603 (Sh za Tanzania trilioni 1.26), sawa na dola 8.61 (Sh 18,081) kwa kila mpigakura.
    Tume ya Uchaguzi Tanzania Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhan Kailima amesema kuna mambo ambayo Tanzania inaweza kujifunza kwa namna ambavyo uchaguzi nchini Kenya umefanyika. Aidha, ameipongeza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) kwa kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 8, mwaka huu na Rais Kenyatta kurejea madarakani akiwabwaga washindani wake saba, akiwemo wa karibu, Odinga.
    “Tume imefanya mambo mazuri sana na wamekuwa mfano hata kuna taasisi zimesema hivyo ikiwemo AU (Umoja wa Afrika) na EU (Jumuiya ya Ulaya), hivyo nina kila sababu ya kumpongeza mtendaji mwenzangu,” alisema Kailima. Alisema utaratibu waliotumia hauna tofauti na utaratibu uliotumika nchini katika uchaguzi mkuu uliopita, lakini kuna baadhi ya mambo yanapaswa kuigwa kutoka kwao. “Mfano matumizi makubwa ya teknolojia, utoaji wa elimu ya mpigakura ambapo wao wameanza kipindi cha maandalizi ya kuboresha daftari la kupigia kura, lakini sisi tutafanya kwa mwaka mzima, kufanya midahalo baina ya Tume na wananchi ili wapate nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa,” alisema Kailima.

    Chanzo habariLeo

    Mbunge Msukuma Kamjibu Tundu Lissu Kuhusu Ndege Kukamatwa Canada Kisa Deni

    By: Unknown On: 11:22
  • Share The Gag
  • Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Msukuma amefunguka na kusema kuwa Rais Magufuli hausiki katika sakata la kuvunja mkataba ambao umepelekea ndege ya Tanzania  Bombadier Q-400 Dash 8 kushikiliwa nchini Canada na kusema wapinzani wanatafuta kiki.

    Mbunge Msukuma amesema kwa upeo wake jinsi alivyosikiliza upande wa upinzani na majibu ya serikali anaona wazi kuwa ni kweli baadhi ya wapinzani wa nchii hii wanahusika katika kukwamisha jambo hilo kama ambavyo serikali ilivyosema na kudai Rais Magufuli hausiki katika jambo hilo.

    "Binafsi yangu naamini kabisa majibu ya serikali kuwa hili suala linauchochezi wa wanasiasa, kwanza vitu vingi walivyosema wapinzani kuhusu sakata hili la ndege ni vya uongo ukianzia lile suala la kuwa Rais Magufuli amekuwa akiiitia hasara serikali hii. 
    "Tatizo lililopo mahakamani la kampuni inayodaiwa kuishtaki Tanzania kampuni hiyo imefanya kazi mwaka 1998-99 wakati Magufuli hakuwa Rais wa Tanzania" alisema Mbunge Msukuma

    Aidha Mbunge huyo aliendelea kudai jumla ya deni la bilioni 87 ambayo serikali ya Tanzania inadaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd kwa kuvunja mkataba wa kazi halijatokana na serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe Magufuli.

    "Deni hili siyo kwamba limetokana na uongozi wa serikali ya awamu ya tano lakini kama Rais huwezi kukataa deni ambalo serikali inadaiwa akiwa madarakani lakini pia suala hili lipo mahakamani na hatua iliyofikia ni hatua ya mwanzo kabisaa, na si kweli kwamba ndege imekamatwa unaweza kuingia mitandaoni ukaiona ndege ilipo, bado ipo kwao hao Bombadier hivyo Tundu Lissu anaposema ndege imekamatwa siyo kweli.
    "Hao watu hao wanaotudai wameenda kufile kesi ya kuzuia mali za Tanzania zisiondoke na serikali inaweza kutoa utetezi wake kwa hiyo hili suala ni kama linawekwa udalali na yote yanafanyika kutokana na umakini wa serikali ya awamu ya tano kwa hiyo wapinzani wanatafuta kiki tu" alisisitiza Msukuma

    Siku ya Jumamosi ya tarehe 19 Agosti serikali ilikiri wazi kuwa ni kweli kuna mgogoro uliopelekea ndege hiyo kushindwa kuingia nchini Tanzania mwezi Julai kama ambavyo ilitangazwa awali na kusema serikali imeanza kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inamaliza mgogoro huo.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Wakuu wa SADC wampongeza Rais Magufuli

    By: Unknown On: 11:20
  • Share The Gag
  • WAKUU wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wamempongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati akiwa mwenyekiti Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya jumuiya hiyo.
    Walitoa pongezi hizo jana wakati wakihitimisha Mkutano wao wa 37 mjini Pretoria, Afrika Kusini. Akizungumzia mambo muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo wa 37 wa SADC, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ambaye alimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, alisema pamoja na mambo mengine, SADC imetambua na kuthamini mchango wa Tanzania katika kipindi cha uongozi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama iliyokuwa chini ya Rais Magufuli.
    Alisema Tanzania imeshakuwa mwenyekiti wa asasi hiyo mara tatu kwa nyakati tofauti, ambapo mara ya kwanza ilikuwa kipindi cha 2006/2007, mara ya pili 2012/2013 na mara ya tatu kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017. Tanzania imemaliza kipindi chake cha Uenyekiti wa Asasi ya SADC Agosti 19, 2017 wakati wa mkutano huo wa 37. Tanzania ilipokea kijiti cha uongozi huo kutoka Msumbiji wakati wa Mkutano wa 36, uliofanyika Swaziland Agosti 30, 2016.
    Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana wakati wa Uenyekiti wa Tanzania katika asasi hiyo ni kusimamia uchaguzi wa Bunge nchini Seychelles, uliofanyika Septemba, 2016. Aidha katika kipindi hicho, Tanzania ilisaidia kurejesha hali ya amani na utulivu nchini Lesotho, ambayo kwa muda mrefu tangu 2014 imekuwa kwenye mgogoro wa kisiasa; pamoja na kushughulikia matatizo ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
    Wakati huo huo, Mkutano huo wa 37 wa SADC ulimuongezea muda mwingine Mtanzania, Dk Stergomena Taxi kuendelea na wadhifa aliokuwa nao wa Katibu Mtendaji wa SADC kwa kipindi cha miaka minne mingine, ambapo atatumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2021. Dk Taxi alithibitishwa jana na Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali na kuapishwa rasmi kushika nafasi hiyo.

    Chanzo HabariLeo

    Jenerali wa Jeshi Ateuliwa na Rais Magufuli Kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

    By: Unknown On: 11:12
  • Share The Gag
  • Raisi John Magufuli leo August 21, 2017 amemteua Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

    Uteuzi wa Brigedia Jenerali John Julius Mbungo unaanza leo August 21, 2017.
     Credit;Mpekuzi Blog