Monday, 5 February 2018

Tiba Asili ya Kuondoa Chunusi, Kupunguza Tumbo, Maziwa Makubwa na Nguvu za Kiume

By: Unknown On: 10:34
  • Share The Gag
  • Asilimia 90 ya wanaume hushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya  kama vile kisukari, punyeto ambayo huathiri mfumo mzima wa wa misuli inayozalisha vichocheo ashiki , kutopata choo vizuri hali ambayo huchakiwa na kula chakula kisicho na asili,tumbo kuunguruma, kujaa gesi,kiuno kuuma, mgongo na miguu kufa ganzi

    SUPER HOLO; Ni dawa itokanayo na miti shamba, ipo katika mfumo wa vidonge na unga. Hutibu na kumaliza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa muda mfupi tu.,SUPER HOLO hurudisha heshima ya ndoa, itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika 15-30. Itakupa hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3. Pia itaimarisha misuli iliyosinyaa na kulegea. Dawa hii hutumiwa kwa watu wa umrii wa miaka 20- 80

    NZOGIWE ni dawaya maumbile.Hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo urefu wa nchi 4-8 na unene wa sentimita 2-4 za upenyo

    NZOGOMA ni dawa asili ya miti shamba, huboresha mbegu za uzazi...huzibua mirija na kusafiisha ili kuweza kushika mimba au kutia mimba.

    Pia tunayo dawa ya kupunguza tumbo, unene, maziwa makubwa, kuongeza hips, makalio na kutoa chunusi

    TUNAPATIKANA MTONI MTONGANI. KANA HAUNA NAFASI YA KUFIKA UTALETEWA ULIPO. WASILIIANA NA DR. MBUSI.  PIGA SIMU NAMBA:   0718 431222
    Credit;Mpekuzi Blog

    Wastara amwaga chozi akiaga kwenda kutibiwa

    By: Unknown On: 10:30
  • Share The Gag
  • Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Wastara ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu ya mguu wake ulioanza kumsumbua mwishoni mwa mwaka jana huku akiwashukuru watanazania na Vyombo vya Habari kwa kuwa pamoja naye kipindi alivyokuwa akihitaji msaada wa fedha.

    Wastara akiongea na waandishi wa Habari jana Jumapili Februari 4, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, alisema “nina washukuru sana vyombo vya habari wote kwa moyo wa upendo walionesha kwa sababu bila ya wao hata mimi nisingekuwa Wastara. 

    "Napenda kuwaambia watanzania kwamba tuamini sana maneno anayosema mtu kuliko neno analosema mtu mwingine kwa hiyo naamini kuna wengine watakuja na matatizo tujaribu kuwaangalia nawao pia”.

    Na alipoulizwa kuhusu tuhuma za kutumia fedha za matibabu kwa starehe kama alivyowahi kuchangiwa kipindi cha nyuma na kwenda Dubai, Wastara alisema hajawahi kuchangiwa na Watanzania bali alisaidiwa na Makamu wa Rais na hakutumia kwa matumizi mengine.

    “Kwanza niseme sijawahi kuchangiwa na Watanzania mimi kama mimi, mara ya kwanza nilipoumwa aliyenichangia asilimia kubwa alikuwa ni Makamu wa Rais, na uzuri ni kwamba mpaka nafika hospitalini nilikuwa nampigia simu. Kilichosababisha watu waseme baada ya kufika hospitali kama hivi ninavyokwambia wiki tatu linapotokea tatizo kama umefanyiwa Oparesheni au upasuaji wowote niliambiwa unauwezo wa kukaa au kuishi kwenye hoteli karibu na hospitali..Ndipo watu wa karibu yangu wa Oman wakawa wamenipa Visa nikaenda kukaa huko kwa muda.“alisema Wastara.
    Advertisement
    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Mgombea udiwani Chadema apatikana akiwa hajitambui

    By: Unknown On: 10:16
  • Share The Gag
  • Mgombea udiwani (Chadema) Kata ya Buhangaza, Mchungaji Athanasio Makoti (28) aliyepotea Februari 2,2018 katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hajitambui.

    Makoti amepatikana leo Februari 5,2018 saa moja asubuhi, Katibu wa Chadema wilayani Muleba, Elisha Kabombo alisema alitelekezwa na watu wasiojulikana jirani na Hospitali ya Kagondo.

    Amesema wananchi waliokuwa wakipita eneo hilo usiku wa kuamkia leo walimuona akiwa kando mwa  barabara ya kuelekea Bukoba, hivyo kumpeleka hospitali.

    “Hali yake si nzuri kwa sababu hawezi kuzungumza vyema wala kuketi. Kawekewa dripu za maji. Tuzidi kumuombea,” amesema.

    Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Isack Msangi amethibitisha kupokea taarifa za kupatikana mgombea huyo. Amesema vyombo vya dola vinamhoji ili kuendelea na uchunguzi.

    Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kagondo, Dk Humphrey Batungi alipoulizwa afya ya mgombea huyo amesema ni mapema kuzungumza.

    “Ninaelekea kwenye kikao nitafute mchana baada ya dawa anazotumia mgonjwa kufanya kazi na huenda akawa na mabadiliko,” amesema Dk Batungi.

    Katibu wa uenezi wa Chadema jimbo la Muleba Kusini na mratibu wa chama hicho jimbo la Muleba Kaskazini, Hamisi Yusufu amesema baada ya kufikishwa hospitali alikutwa na majeraha, huku akizungumza kwa shida.

    Amesema mgombea huyo wa udiwani aliwaeleza amenyang’anywa fedha, waliomteka walimfunga kitambaa cheusi usoni na kumtaka asigombee uchaguzi utakaofanyika Februari 17,2018 na amekiri  kuwafahamu baadhi ya waliomteka.

    Katika uchaguzi huo anachuana na mgombea wa CCM, Jenitha Tibeyenda na wa NCCR-Mageuzi, Grason Anaseti.


      Credit; Mpekuzi Blog 

    Mwanasheria Mkuu wa Serikali Aapishwa Rasmi Bungeni

    By: Unknown On: 10:14
  • Share The Gag
  • Naibu Spika wa Bunge, Dkt.  Tulia Ackson amemwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dkt. Adelardus Kilangi bungeni na kumkabidhi vitendea kazi kabla ya kuanza kwa Kikao cha Tano cha Mkutano wa 11 wa Bunge, Mjini Dodoma, leo Feb 5, 2018.
     
    Dkt. Kilangi ambaye amekula kiapo cha uaminifu, aliteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Mgufuli,  Februari Mosi, 2018 na Paul Ngwembe aliteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

    Katika hatua nyingine,Magufuli alimtea aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na naibu wake, Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambao waliapishwa juzi Jumamosi, Ikulu jijini Dar es Salaam.




      Credit; Mpekuzi Blog 

    Watumishi Wasiyoiunga Mkono CCM Kufukuzwa Kazi

    By: Unknown On: 10:13
  • Share The Gag
  • Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amefunguka na kuwataka watumishi mbalimbali mkoani kwake ambao hawaiungi mkono Serikali ya awamu ya tano iliyopo chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuondoka mapema katika nafasi zao hizo.

    Mnyeti amesema kuwa siku zote Chama Cha Mapinduzi ndiyo kimekuwa kikihangaika kuomba kura majukwaani huku viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwa si wanufaika wakubwa kulinganisha na watumishi, hivyo watumishi wanapaswa kutambua na kuiunga mkono Serikali ya CCM na kama hataki waondoke kwenye nafasi hizo.

    "Wanaoumia kuomba kura majukwaani ni CCM anayekuja kula ugali na familia yake ni wewe mtumishi, unanufaika wewe na familia yako. Sasa tumejipanga vizuri wale wote ambao siyo wenzetu watupishe mapema kabla ya uchaguzi, mimi ndiyo Mkuu wa Mkoa huu wa Manyara nasema hivi kama wewe huungi mkono Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ondoka mapema" alisisitiza Mnyeti
    Credit; Mpekuzi Blog

    Monday, 22 January 2018

    'Nabii Titto' Ajitokeza, Aanika Kuhimiza Bia Madhabahuni, Akomaa Kumuoa Wema Sepetu

    By: Unknown On: 10:09
  • Share The Gag
  • Mkazi  mmoja wa Dodoma anayejitangaza kama nabii, Tito Machija amesema watu wasimuone kuwa hana akili kutokana na mahubiri yake ambayo yanatofautiana kwa kiasi kikubwa na imani za waumini wa dini nyingine, hasa Wakristo.

    Machija, ambaye anajulikana kama ‘Nabii Tito’ anahamasisha kuoa mke zaidi ya mmoja, ikiwa ni pamoja na kutembea na wafanyakazi wa ndani; anatumia pombe kunasa waumini na anadai hataki nyimbo za injili kwenye ‘ibada’ zake, ambazo nyingi hufanyikia baa.

    ‘Nabii’ huyo anaonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa amevalia kanzu nyeupe yenye misalaba miwili, chupa ya bia na kitabu kitakatifu aina ya Biblia.

    “Nawashangaa wanaoniona mimi sina akili, niko timamu kabisa na ninaelewa ninachokifanya,” alisema.

    “Narudia tena kusisitiza kuwa walevi ndio watakaoingia ‘mbinguni’ na mafundisho ninayoyatoa ni sahihi,”

    Tito amekuwa akionekana kwenye mitandao ya kijamii, hususani kwenye video fupifupi za Instagram, akiwa amevalia mavazi kama ya kichungaji na kucheza muziki huku akinywa bia na akiwa ameshika biblia.

    ‘Nabii’ huyo, mwenye wake watano na watoto 12, amedai kuwa kwa sasa hitaji lake kubwa ni kumuoa mwigizaji Wema Sepetu ili aungane naye katika huduma zake.

    “Wema ni msichana mzuri wa sura na umbo nataka nimuoe awe sehemu ya kanisa langu na nina imani watu wengi wataongezeka kwenye ibada ili kuja kumuona yeye na wake zangu hawana tatizo na hilo hata mmoja wao ananisaidia kumshawishi ili tuungane naye,” alisema Tito.

    Tito anakiri kuwa ‘kanisa’ lake halijasajiliwa ila anadai kwamba anapata ufadhili kutoka kwa walevi mbalimbali.

    Tito amedai  kuwa ‘kanisa’ lake lipo karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma na mara nyingi ibada zake huwa anazifanya kwenye baa na ana wafuasi  wengi kiasi cha kutojua  idadi yao.

    Amesema kabla ya ibada kufanyika kwenye baa husika, huanza kwa kupeleka vipeperushi kwa mmiliki ili kuwapa taarifa waumini wake siku hasa ya ibada kufanyika katika baa hiyo.

    “Siku ya ibada ikifika naenda pale nikiwa na bia zangu za (anaitaja aina ya bia) ambazo nimeshaziombea. Zina ‘upako’. Kila anayetaka kuingia kwenye ibada analipa kiingilio cha Sh12,500. Ukilipa pesa hiyo unapata bia zako tano ndiyo huduma inaendelea usipotoa unafukuzwa,” alisema.

    Tito anajinasibu kuwa ana waumini wengi ambao hujitokeza kusikiliza mafundisho yake ambayo kwa kiasi kikubwa yanahamasisha ulevi na mapenzi kwa wasichana wa kazi wa majumbani.

    Amesema kwenye huduma zake nyimbo za injili hazina nafasi kwa kuwa huwaburudisha waumini wake kwa nyimbo za kisasa.

    “Mtu akishaweza safari zake kichwani ukimuwekea bongofleva anacheza na kufurahi huku ibada inaendelea,” alisema.

    Nabii huyo amedai kuwa hakuna anachokizungumza kutoka kichwani mwake bali anasimamia mistari ya vitabu vitakatifu.

     “Wapo wengi wanaopinga huduma zangu ila nawaambia sijakurupuka nafanya kitu ambacho kipo na wala sioni kama ninakosea,” alisema.

    Kwanini ‘ibada’ kwenye baa
    Tito amedai kuwa anaingia makubaliano na wenye baa kwa kuwa ndiyo sehemu ambayo walevi hukutana na kwake ni mahali sahihi pa kutoa huduma.

    “Pale nakwenda na bia zangu kadhaa kwa ajili ya waumini watakaoingia kwenye ‘ibada’. Zikiisha naondoka zangu, nawaacha wanaendelea kununua za baa hapo ndipo mwenye baa anaponufaika,” alisema.

    Watu wengi wamekuwa wakilaumu mafundisho ya Tito kuwa yanapotosha na wameiomba Serikali kuchukua hatua.
    Credit: Mwananchi


    ==
    Credit Mpekuzi Blog