Tuesday, 27 September 2016

Baada ya kuzushiwa kifo, Bilionea Dangote ameyaandika haya

By: Unknown On: 01:44
  • Share The Gag
  • Bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote amekanusha uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia akiwa nchini Ujerumani.

    Taarifa hizo zinaeleza kuwa bilionea huyo amefariki akiwa nchini Ujerumani baada ya kuugua kwa muda mfupi. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa familia ya bilionea huyo imethibitisha kifo cha ndugu yao huyo na kusema kuwa ni pigo kubwa kwa Afrika.

    Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dangote ameandika hivi “I am hale, hearty and alive. Please disregard malicious report saying otherwise. Thank you.” , akimaanisha kuwa yeye ni mzima wa afya na kuwataka watu kupuuzia taarifa zinazoeleza kivingine.”

    Akimaanisha “Mimi ni mzima na buheri wa afya. Tafadhali puuzeni taarifa zote zinazosema vinginevyo. Asanteni.”

    Aliko Dangote ni raia wa Nigeria, ndiye mwenye utajiri mkubwa zaidi barani Afrika. Dangote anamiliki kampuni kubwa ya Dangote Group inayofanya kazi katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwa ni pamoja na Nigeria, Benin, Ethiopia, Senegal, Cameroon, Ghana, Afrika Kusini,  Togo, Tanzania na Zambia.
    Muda mfupi baada ya kuzuka kwa taarifa hizo, Aliko Dangote alikanusha taarifa hizo kupitia mtandao wa Twitter kwa kupost kuwa yuko Afrika kusini na yuko salama kabisa.


    Credit; "UDAKU SPECIAL"

    Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam Degree-2016/2017

    By: Unknown On: 01:31
  • Share The Gag

  • The following applicants have been selected to join various undergraduate degree programmes for the 2016/2017 academic year. 
    The selected applicants should report at the Mwl. J.K. Nyerere Mlimani Campus on Saturday 8th October 2016 for the orientation week which will start on Monday 10th October 2016. 
    Applicants selected for admission into Dar es Salaam University College of Education (DUCE) and Mkwawa University College of Education (MUCE) should report directly to the college's campuses in Chang'ombe and Iringa respectively on the same dates. 
    Joining instructions and admission letters should be collected at the University campuses where one is admitted. Joining instructions and other important information can also be downloaded from the University website.


    Credit; "UDAKU SPECIAL"

    List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017

    By: Unknown On: 01:29
  • Share The Gag

  • Kuona Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Chuo Kikuu 2016/2017,
     

    ==>Chuo  Kikuu Cha Mwalimu Nyerere   <<bonyeza Hapa>>==>Chuo  Kikuu Cha  Udsm,duce Na Muce   <<bonyeza Hapa>>==>Chuo  Kikuu Cha  Tumaini Makumira    <<Bonyeza Hapa>>   

    ==>Chuo  Kikuu Cha Udom  <<bonyeza Hapa>>

     ==>Chuo  Kikuu Cha Ifm <<bonyeza Hapa>>

    ==>Chuo Kikuu Marian << Bonyeza Hapa>>

     ==>Chuo Kikuu Cbe        << Bonyeza Hapa>>

    ==>Tumaini-mbeya     << Bonyeza Hapa>> & <<hapa>>

     ==>Chuo Kikuu Mum         << Bonyeza Hapa>>

    ==>Chuo Mum(Diploma) <<Bonyeza Hapa>>

     ==>Chuo- Stella Maris   << Bonyeza Hapa>>

     ==>Chuo- Kampala-kiu  << Bonyeza Hapa>>


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Saturday, 17 September 2016

    Simba, Azam Hapatoshi.. Warushiana Tambo Mechi ya Leo Ligi Kuu Bara

    By: Unknown On: 00:55
  • Share The Gag
  • Michuano ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena leo ambapo Simba na Azam FC zinazotarajia kukutana kwenye Uwanja wa Uhuru zimeelezea kuhusu mchezo huo.

    Afisa Habari wa Simba SC Haji Manara amesema, kikosi kimejiandaa vizuri kwa ajili ya kuweza kupambana na wanauchukulia huo kama michezo mingine hivyo wanaamini wataweza kuvuna pointi tatu mbele ya Azam FC.

    Manara amesema, mpaka sasa wana majeruhi wawili pekee ambao ni mshambuliaji Ibrahim Ajibu na kiungo Mwinyi Kazimoto ambao daktari anaendelea kuangalia hali zao kama wataweza kucheza mchezo wa kesho au bado wataendelea kuwa katika uangalizi.

    Kwa upande wake Afisa Habari wa Azam FC Jafary Iddy Maganga amesema, mchezo huo utakuwa na changamoto kubwa kutokana na wote kuwa na pointi sawa katika msimamo wa ligi lakini watapambana ili kuhakikisha wanashinda huku akiwataka waamuzi wa mchezo huo kusimamia sheria 17 za soka ili kuhakikisha timu inashinda kutokana na uwezo wake.

    Maganga amesema, kwa upande wao majeruhi ni walewale ambao walikuwa nao katika mchezo dhidi ya Mbeya City ambao ni mshambuliaji Gonazo Bi Thomas, Beki Erasto Nyoni na Agrey Morris pamoja na Mlinzi wa kati Paschal Wawa.

    Michezo mingine itakayopigwa hapo kesho ni Mtibwa Sugar wakiwakaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Manungu Mkoani Morogoro, Mbeya City akiwakaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya, Mwadui FC akiikaribisha Yanga Uwanja wa Mwadui Mjini Shinyanga na Ruvu Shooting akiikaribisha Mbao FC Uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani


    Credit; UDAKU SPECIAL

    Meneja Wa Diamond Platinums Afunguka Kuhusu Ali Kiba Kufanya Show Kwa Kushtukiza Jukwaa Moja Na Diamond Platinums Kenya

    By: Unknown On: 00:53
  • Share The Gag
  • Meneja wa Diamond azungumzia Ali Kiba kufanya show kwa kushtukiza kwenye jukwaa moja na Diamond Kenya..

    International Meneja wa Diamond Platnumz ‘Sallam Sk’ ameongea na Sammisago Kupitia ENews leo kuhusu Ali Kiba kufanya show kama msanii wa kushtukiza kwenye jukwa moja na Diamond Platnumz.

    Sallam anasema “Sisi hatukuambiwa kama Ali Kiba atakuwepo kwenye show kwa hio Ali Kiba alikuwa kwenye show kama Suprise, nashukuru muziki wetu wa Tanzania unazidi kukua,

    tulichofanya ni kitu mkataba wetu umesema tufanye , na tuliperform kwa saa mbili, hawakuandika Diamond is a Tanzanian artist, ila waliandika International Artist, kama alitangazwa Diamond pekee yake, akaje msanii mwingine pia hio ni sawa tu”

    Hii ni hatua nyingine inayothihirisha kuwa ladba hakuna beef kati yao na kwamba wote wanakubalika kama wasanii wa kimataifa….


    Credit; UDAKU SPECIAL

    UTAFITI:Faida za Kiafya Kwa Wanawake Wenye Makalio Makubwa Hizi Hapa

    By: Unknown On: 00:52
  • Share The Gag

  • Licha ya mvuto yaliyonayo yakiwa kwenye jinzi, makalio makubwa ya wanawake ni kinga kwa kisukari na magonjwa ya moyo.

    Wataalamu wa afya wanadokeza kwamba makalio ni muhimu kwa afya ya binadamu kwani huwezesha kusimama na kutembea vile anavyoonekana. Na cha pekee, hueleza afya ya mtu hasa mwanamke.

    Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza unaeleza uhusiano uliopo baina ya mwonekano wa makalio ya mwanamke na hatari yake ya kupatwa na magonjwa hayo kwa kuzingatia mgawanyo wa mafuta mwilini.

    Majibu ya utafiti huo yanaeleza kuna uhusiano wa karibu kati ya mgawanyo wa mafuta mwilini na afya ya mwanamke ingawa mafuta hayo hayasambazwi kwa usawa kwenda sehemu tofauti za mwili.

    Kiasi kikubwa cha mafuta kikihifadhiwa kwenye matiti ni hatari kwa afya kwa sababu yapo karibu na moyo kwani huongeza uwezekano wa kuziba kwa mishipa ya damu, lakini makalio ya wastani yanaashiria siha njema.

    Utafiti huo ulibaini uvungu wa makalio hasa sehemu za juu za mapaja na nyonga ndiko yanakohifadhiwa mafuta ya ziada au fatty acids ambayo ni kinga dhidi ya magonjwa hivyo mhusika kuwa na afya njema.

    “Mafuta yasipohifadhiwa sehemu salama huenda kwenye ini au mishipa ya damu ambako huweza kusababisha kisukari au magonjwa ya moyo,” anasema Dk Konstantinos Manolopoulos, kiongozi wa utafiti huo.

    Ipo tofauti kati ya mwanamke na mwanaume kuhusu usambazaji wa mafuta mwilini.

    Inaelezwa kwamba wanawake wanahifadhi zaidi mafuta sehemu ya chini ya mwili; mapaja, nyonga na makalio kuliko wanaume.

    Hii ni habari njema kwa wanawake na wasichana ambao bado wanapata siku zao kwani kwa mujibu wa Dk Manolopoulos, kuwa mwanamke mwenye homoni za kike ni kinga ya magonjwa ya moyo kwa kiasi fulani. Lakini baada ya kukoma kwa hedhi, homoni hubadilika.

    “Mwonekano wa kike unapotea na badala yake kitambi huanza kujitokeza. Badala ya mafuta kwenda makalioni, sasa yanahifadhiwa tumboni hivyo kuongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya magonjwa hayo hivyo kuwa sawa na wanaume wa umri huo,” anasema huyo.

    Utafiti wa awali uliofanywa mwaka 2008 na kuchapishwa kwenye International Journal of Obesity kwa kutumia panya ulionyesha kwamba licha ya mafuta yanayohifadhiwa tumboni kuyeyushwa kwa urahisi, ni hatari kwani huziba mishipa ya damu na kurahisisha mshtuko wa moyo.

    Ingawa hakuna uhakika wa namna mwili unavyogawanya hifadhi ya mwilini, watafiti hao wanabainisha kwamba watu wenye makalio makubwa wana nafasi ndogo ya kupata maradhi hayo hata watakapozeeka.

    Dk Benjamini Rulakuze wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), anasema unaunga mkono utafiti huo na kufafanua kuwa magonjwa ya moyo na kisukari husababishwa na wingi wa mafuta katika mwili.

    Dk Rulakuze anasema sehemu za tumbo, matiti, mapaja na makalio ndiyo hutumika zaidi kuhifadhi mafuta kwa mwanamke na endapo mtu atakuwa na mafuta mengi yanaweza kuathiri mishipa ya damu kwani hurundikana na kuifanya mishipa ya damu kuwa miembamba na kuzuia damu kupita kwa urahisi hali inayorahisisha shinikizo la damu.

    Anasema: “Mafuta huathiri ufanisi wa kongosho kuzalisha homoni ya insulini ambayo hutumika kusafirisha sukari ya mwili kwenda kwenye seli za mwili ili zitumike kuupa mwili nguvu.”

    Anasema endapo sukari itashindwa kuingia katika seli za mwili na kuyeyushwa, mtu anaweza kupata kisukari aina ya kwanza na ya pili.

    Na endapo mafuta yatakuwa mengi yanaweza kubadili oksijeni iliyokuwa itumike kusafirisha glucose na kufanya seli zishindwe kupokea sukari hiyo, hivyo kuibakiza sukari kwenye damu na kusababisha ongezeko la sukari katika damu.

    Daktari huyo anaeleza kuwa mbali na wanawake, wanaume ambao hupata matatizo ya kisukari na magonjwa ya moyo ni kutokana na mafuta mengi katika tumbo na kusababisha kitambi ambavyo wengi wetu hudhani kuwa ni afya.

    “Endapo mafuta hayo yataongezeka zaidi huathiri mfumo wa damu kwa kuziba mishipa hivyo kuinyima nafasi ya kutosha kupita na kusababisha shinikizo la damu,” anasema.

    Anaeleza kuwa ili kuepukana na matatizo hayo ni vema mtu akafanya mazoezi kila wakati ili kujiweka sawa na kupunguza mafuta mwilini. Mazoezi hayo yanaweza kuwa ni kukimbia, kukata tumbo na mengine ambayo husaidia kupunguza mwili.

    Mbali na mazoezi ameshauri kuwa makini na matumizi au ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi kama nyama na kupendekeza matumizi ya mafuta ya mimea.

    Daktari mwingine, Eliza Wampembe wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (Muhas) anasema mbali na sababu hizo, kisukari kinaweza kurithiwa kutoka kwa wazazi au wanafamilia wengine ambao walikuwa na ugonjwa huo ndani ya ukoo.

    Dk Eliza anabainisha kuwa mgonjwa wa moyo na kisukari yupo hatarini kuathirika na maambukizi mengine kwani huathiri figo na kongosho, hivyo kupunguza kinga za mwili.

    “Miongoni mwa athari za kisukari ni miguu kuwa na vidonda visivyopona kwa urahisi kiasi cha kukatwa kwa baadhi ya wagonjwana kusababisha ulemavu ambao hawakuzaliwa nao,” anasema.

    Pia, shinikizo la damu husababisha matatizo ya figo, macho, kiharusi, misuli ya tumbo na kutosikia vizuri.

    Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2015 ya Shirikisho la Kisukari (IDF) Afrika, zaidi ya watu milioni 14 barani humo wana ugonjwa huo na idadi inaweza kuongezeka hadi kufikia milioni 34 mwaka 2040 endapo jitihada za dhati za kukabiliana nao hazitachukuliwa.

    Ripoti hiyo inasema asilimia 66.7 ya watu wote barani Afrika wana kisukari, kati yao asilimia 79 ni wenye umri zaidi ya miaka 60.

    Ripoti imeeleza ugonjwa huo ulisababisha zaidi ya vifo vya watu 300,000 mwaka 2015.

    Licha ya mikakati ya Serikali kukabiliana na magonjwa mbalimbali, wataalamu wa afya wanashauri kila mwananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari zinazotolew


      Credit;UDAKU SPECIAL

    Lipumba, Sakaya, Kambaya watuhumiwa kupanga njama za utekaji viongozi wa CUF

    By: Unknown On: 00:01
  • Share The Gag
  • Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha ambaye pia ni Kaimu Naibu Mkuu CUF, Bara Joran Bashange
    Chama cha Wananchi (CUF) kinawatuhumu waliokuwa viongozi wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho na Magdalena Sakaya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Bara kufanya jaribio la kumteka Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha ambaye pia ni Kaimu Naibu Mkuu CUF, Bara Joran Bashange.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma CUF inadai kuwa jana majira ya 2:30 asubuhi vijana wanaosadikiwa kuwa wa Prof Lipumba wamefanya jaribio la kutaka kumteka Bashange wakati akitoka nyumbani kwake eneo la Buguruni.

    Na kwamba watekeji hao wakiwa na gari aina ya Noah yenye namba ya Usajili T 760 CEX  baada ya jaribio la kumteka, walifanikiwa kumuingiza katika gari hiyo ya NOAH iliyokuwa na vioo vyeusi (tinted).

    Taarifa hiyo ilieleza kuwa Bashange alipambana na kuomba msaada kwa kuita watu waliojirani kwa yowee la kuita “Majambazi” ndipo wananchi wakalizingira gari hilo na kuweka mawe na magogo na kuita Polisi.

    Baada ya Polisi kufika waliwakagua vijana hao na kuwakuta na pingu, silaha kadhaa na kitambulisho feki cha polisi.

    Baada ya ukaguzi kufanyika vijana watatu walikamatwa na mmoja alifanikiwa kukimbia.

    Taarifa hiyo ilifafanua kuwa mmoja kati ya vijana waliokamatwa ni mlinzi wa karibu wa Prof. Lipumba aitwaye HAJI “Mrangi” ambaye ni maarufu na anadaiwa kujulikana kwa ushiriki wake wa vitendo vya kihuni na kiharamia kama hivyo.

    Hata hivyo, katika mahojiano ya awali mmoja wa vijana hao alitoa ushirikiano na kueleza kuwa wametumwa na Abdul Kambaya na kwamba anayeongoza oparesheni yao hiyo ni mtu aitwaye Athumani (Mganga wa Kienyeji na Mwalimu wa mafunzo ya Kareti) aishiye Ilala akisaidiwa na watu wengine wanaojulikana Abubakar Fambo, Mohamed Ibrahim na Hassan Kingwele ( Mlinzi wa Magdalena Sakaya (MB).

    Vijana hao waliokamatwa wanakiri kuwa mipango yote hiyo Prof. Lipumba anaijua kama vile walivyoongoza mpango wa kuhujumu Mkutano Mkuu Maalumu wa CUF ulioahirishwa pale Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza.

    Joran Bashange ameumizwa maeneo kadhaa ya mwili na anaendelea na matibabu na taarifa za ndani zinaonesha kuwa wahusika walielekezwa kumshambulia vibaya na kumuua ikiwa wangelifanikiwa kuondoka naye.

    Vijana waliohusika na utekaji huo na gari lao wanashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Polisi Buguruni.

    Chama cha CUF kimelaani kitendo hicho na kimesema kinachukua hatua stahiki.

    Pia Chama hicho kimesema kinaamini kuwa kwa sasa Prof. Lipumba na watu wake wamekusudia kuendesha hujuma za wazi na kuvuka mipaka ya ushindani wa kisiasa za ndani ya Chama na kujivika joho la ‘Uintarahamwe na Umungiki’ wa wazi dhidi ya Chama na kuhatarisha na kutishia usalama wa maisha ya viongozi wa Chama.


    ==

    cREDIT Mpekuzi Blog

    Friday, 16 September 2016

    Shilole Aeleza Kilichomsukuma Kupatana na Nuh Mziwanda

    By: Unknown On: 23:53
  • Share The Gag

  • Baada ya hivi karibuni Sholole na Nuh Mziwanda kupatana, Shilole amefunguka na kuzungumzia nini kimemsukuma mpaka akapatana na mkali huyo wa wimbo ‘Jike Shupa’.
    Wawili hao ambao walikuwa wapenzi waliachana kwa kutupiana maneno huku Nuh Mziwanda akionekana kumlaumu Shilole kwa kumpotezea muda.

    Akiongea na Uhead ya Clouds FM Ijumaa hii, Shilole amedai ameamua kumaliza tofauti zake na Nuh Mziwanda kwa kuwa muimbaji huyo wa ‘Jike Shupa’ alikuwa anapoteza kujiamini pale anapokutana naye.

    “Nikwambia kitu situation moja ambayo ipo, Nuh akiniona mimi huwa anapoteza kujiamini,” alisema Shilole. “Sasa ili kumueka sawa na aweze kuwa vizuri lazima na mimi nimwonesha am good. Kwa hiyo alivyoniona nipo good na yeye akawa fresh na furaha imerudi na nazani maisha yanaendelea,”

    Hata hivyo mkali huyo wa wimbo ‘Say My Name’ alikanusha kurudiana na Nuh Mziwanda huku akidai kwa sasa wao ni washkaji.


    Credit; UDAKU SPECIAL

    Wanaowapigia simu polisi bila sababu Kuchukuliwa Hatua za Kisheria

    By: Unknown On: 23:48
  • Share The Gag
  • JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limeahidi kuwachukulia hatua kali wananchi wanaotumia vibaya simu za dharura, zenye namba 111 na 112.

    Simon Sirro, Kamishina wa Jeshi la Polisi amesema kuwa watu wamekuwa wakipiga simu hizo na kutoa taarifa za uongo au kupiga simu na kisha kuwapa watoto wadogo waongee.

    “Polisi tutawafuatilia wote kupitia mitandao yetu General Packet Radio Service (GPRS),inayoonyesha maeneo walipo na simu wanazotumia ili kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria. Haiwezekani mtu apige simu halafu baada ya simu kopokelewa anaweka muziki,” amesema.

    Kamanda Sirro amesema ni vyema wananchi wakaacha mzaha na matumizi ya namba hiyo ya Jeshi la Polisi kwani kwa kufanya hivyo inapunguza morali ya askari wa jeshi hilo kufanya kazi kwa kujituma.

    “Wananchi wote watumie simu zetu kutoa taarifa zenye ukweli na zitafanyiwa kazi kwa wakati, wawasiliane na sisi pale wanapoona viashiria vya uhalifu ama tukio lolote linaloleta uvunjifu wa amani na siyo kupiga simu na kufanya mzaha,” amesema Sirro.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    UKUTA Waiponza Redio ya Lowassa....Yafungwa Kwa Miezi 3 na Faini ya Milioni 5

    By: Unknown On: 23:45
  • Share The Gag
  • Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia Kamati yake ya Maudhui imekifungia kituo cha Redio 5 Arusha kwa kipindi cha miezi mitatu pamoja na kukitoza faini ya sh. Milioni 5 kwa kosa la kukiuka baadhi ya Kanuni za Huduma za Utangazaji (maudhui) kupitia kipindi chake cha Matukio kilichorushwa Agosti 25, 2016.

    Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo, katika kipindi hicho Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mh. Godbless Lema alitamka maneno ya kashfa yaliyolenga kumdhslilisha Rais John Magufuli na serikali kwa ujumla.

    Wakati akisoma maamuzi ya kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Joseph Mapunda, aliongeza kuwa kituo hicho pia kilirusha maneno yaliyo tamkwa na Lema ambayo yalikuwa yakihamasisha wananchi kushiriki katika maandamano ya Ukuta yaliyopigwa marufuku na Jeshi la Polisi.

    “Maneno ya Lema yalilenga kuhamasisha wananchi kupambana na jeshi la polisi na hivyo kusababisha uvunjifu wa amani na kuhatarisha usalama wa Taifa,” alisema.

    Mapunda alisema uamuzi huo umetolewa na kamati hiyo baada ya kamati hiyo kusikiliza maelezo ya utetezi yaliyotolewa na wa Uongozi wa Redio 5 Arusha.

    “Baada ya kusikiliza maelezo ya utetezi kamati imeridhia kuwa kipindi cha matukio kilikiuka baadhi ya kanuni za maudhui namba 5(a,b,c,d,f,h) 6(2) (b, c) na 18 (1) (b),” alisema.

    Aliongeza kuwa ” kituo hicho kinatozwa faini ya sh. Milioni 5 ambazo zitatakiwa kulipwa ndani ya siku 30 kuanzia leo, kinafungiwa kwa miezi 3 na kuwekwa chini ya uangalizi maalumu kwa muda wa Mwaka 1 baada ya kipindi cha kufungiwa kumalizika, “

    Hata hivyo, Mapunda alisema haki ya wahusika kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo iko wazi ndani ya siku 30 kuanzia leo.

    Kwa upande wa kituo cha redio cha Magic Fm ambacho nacho pia kwa mujibu wa kamati hiyo kinadaiwa kukiuka kanuni za maudhui kupitia kipindi chake cha Morning Magic kipengele cha Paka Rangi ambapo kilirusha maneno yanayodaiwa kumkejeli rais na wananchi, kimepewa onyo kali pamoja na kutakiwa kuomba radhi kwa muda wa siku tatu mfululizo.

    “Baada ya kusikiliza na kutafakari kwa kina maelezo ya utetezi yaliyotolewa na Uongozi wa Magic Fm Redio, Kamati ya Maudhui imeridhika kuwa kipindi cha Morning Magic kilikiuka baadhi ya kanuni za huduma za utangazaji 2005. Kamati ya maudhui inaamua kutoa onyo kali kwa Magic Radio, ” alisema na kuongeza.

    “Pia inatakiwa kumuomba radhi Rais John Magufuli, wasikilizaji na wananchi kwa ujumla. Tangazo la kuomba radhi litolewe kwa siku tatu mfululizo katika taarifa za habari za saa 10.00 alasriri, na 3.00 usiku kuanzia tarehe 17,9,2016.”


    ==

      Credit; Mpekuzi Blog