Saturday, 15 April 2017

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Aman Mwasote Ahukumiwa Kifungo cha Nje cha Miezi 6

By: Unknown On: 01:04
  • Share The Gag
  • Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, imemuhukumu kifungo cha nje cha miezi sita na kulipa faini ya Sh1 milioni, Aman Mwasote baada ya kutiwa hatiani kwa kumwita mtoto wa miaka tisa kuwa mchawi.
     
    Mwasote, ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili alishtakiwa kwa kutoa kauli kuwa mtoto huyo huwaloga wanafunzi na walimu alipokuwa kwenye mkutano wa injili.
     
    Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi, Venance Mlingi aliyesema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa Jamhuri kwamba, Mwasote alitenda kosa hilo.
     
    Awali, Wakili wa Serikali, Xaveria Makombe alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 20, mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Kalobe, akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Injili.
     
    Hakimu Mlingi alisema mshtakiwa atatumikia kifungo cha nje kwa kufanya shughuli za kijamii na Aprili 20 atatakiwa kufika mahakamani ili apangiwe shughuli ya kufanya.

    Advertisement
    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    CM Wamteua DR Gertrude Rwakatare Kuchukua Nafasi ya Sophia Simba Aliyefukuzwa

    By: Unknown On: 01:00
  • Share The Gag

  • Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatare ameteuliwa kuwa Mbunge Viti Maalumu(CCM) kuchukua nafasi ya Sophia Simba aliyefukuzwa uanachama.

    Ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza Mchungaji Rwakatare alipata nafasi kama hii katika Bunge lililopita.

    Uteuzi huu umekuja baada ya Spika wa Bunge kuiandikia barua ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) na kuiarifu juu ya uwepo wa nafasi ya Ubunge Maalum kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) baada ya Sophia Simba kupoteza sifa za kuwa Mbunge baada ya kuvuliwa uanachama.
     
    Credit; Udaku Special.
    By: Unknown On: 00:48
  • Share The Gag
  • Ndoa ya Lulu na Boss wa EFM Majay yanukia



    Elizabeth Michael (Lulu) amedai ndoa yake na mpenzi wake Dj Majay inakaribia.

    Muigizaji huyo ambaye ameonekana kutulia sana tangu alipokuwa na mahusiano na bosi huyo wa EFM na TVE amesema hivi karibuni wale waliokuwa wakitaka waachane watabaki midomo wazi. “Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo wa Mungu. Hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni,” ameliambia gazeti la Mtanzania.

    Lulu ameongeza kuwa anatamani kuwa mke bora kwenye ndoa yake kama alivyokuwa sasa kwenye mahusiano yake.
     
     TOA MAONI YAKO HAPA
     
    Credit; Udaku Special.
     
    By: Unknown On: 00:43
  • Share The Gag
  • Kauli ya Mwigulu Nchemba baada ya kutembelea eneo walilouawa askari 8

    WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi,Mwigulu Nchemba,amesema hawatokubaliana na mtandao,kundi ama mtu anaehusika na kugharimu maisha ya askari ama wananchi wasio na hatia.

    Aidha amebainisha kwamba kilichombele kwa sasa ,wanaendelea kuhakikisha kuwa wanarudisha silaha zinazochukuliwa katika matukio mbalimbali ya mauaji ya askari na kuendelea na mapambano na wahalifu hao.

    Nchemba ameyasema hayo jana  ,wilayani Kibiti,mkoani Pwani,na kumtaka mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo kupambana na matukio ya mauaji yanayoendelea katika baadhi ya wilaya mkoani hapo.

    Waziri huyo wa mambo ya ndani ,alieleza kwamba,amepokea taarifa ya kuuwawa kwa askari nane wilayani Kibiti  kwa mshituko mkubwa .

    Nchemba aliwaomba watanzania kwa kipindi hiki wawe watulivu wakati jeshi la polisi likiendelea kukabiliana na mambo hayo.

    “Hii ni changamoto kwa wizara ya mambo ya ndani kuanza upya kuboresha mbinu zake za ki intelensia zinazoendana na mazingira ya sasa kwa mahitaji ya sasa”alisema.

    Alibainisha kwamba,ni ngumu kuingia akili kwa watu wachache kuuwa hovyo askari ambao ndio walinzi wa raia na mali zao

    “Kuna jambo lipo nyuma limejificha ambalo mwisho wake umefika kwani hatutoweza kulifumbia macho”alisisitiza.

    Nchemba aliomba jamii iendelee kulinda amani ya nchi na kuheshimu askari polisi ambao wapo kwa ajili ya kuwalinda katika usalama wao.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog