Wednesday, 20 July 2016

BAVICHA Waikimbia Dodoma......Waamua Kuhamishia Mkutano wao Dar es Salaam

By: Unknown On: 02:53
  • Share The Gag
  • Wakati kukiwa na ulinzi mkali mjini Dodoma kuelekea Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limehamishia mkutano wake wa kamati ya utendaji jijini Dar es Salaam.

    Jana, sekretareti ya CCM ilianza maandalizi kusafisha njia kwa ajili ya kikao cha Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na baadaye Mkutano Mkuu uliopangwa kufanyika Jumamosi.

    Awali, Bavicha ilikuwa imehamasisha vijana wa chama hicho kuja kwa wingi mjini hapa kwa ajili ya “kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa”, lakini Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alifuta mpango huo akisema: “Waache wafu wawazike wafu wao”.

    Pamoja na Mbowe kuzuia, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi alisema wiki iliyopita kuwa wameandaa mkutano wa Kamati ya Utendaji wa Baraza hilo leo mjini Dodoma na ungefunguliwa na Mbowe.

    Huku ulinzi ukizidi kuimarishwa, jana kulikuwa na uamuzi tofauti.

    Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Dodoma, Malambaya Manyanya jana alisema wameamua kuuhamishia mkutano huo Dar es Salaam baada ya kuona mzozo umekuwa mkali.

    "Tumeona mzozo ni mkali sana. Tumeona imeshakuwa shida, tukaona ngoja tukafanyie Dar,” alisema Manyanya.

    Alisema wajumbe waliokuwa waingie Dodoma jana, wameambiwa wote waelekee Dar es Salaam  kwenye jengo la makao makuu

    Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka yeye anasema kutakuwa ulinzi mkali na hakuna atakayeweza kujaribu kuvuruga mkutano huo ambao utashuhudia Rais John Magufuli akichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho.

    Ole Sendeka alisema kwenye ukumbi mpya wa CCM ambako ndiko mkutano huo utakafanyika, kutakuwa na kamera maalumu zitakazofungwa ndani na nje ya ukumbi ili kuwezesha kuona kila kitu kinachoendelea.

    Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, alisema ameona kwenye mitandao ya kijamii kwamba baadhi ya vyama vinatoa vitisho na kuwataka wananchi wavipuuze.

     “Na kama kuna mtu anadhani kuwa anaweza kukwamisha mkutano mkuu wa CCM, nimwambie Dodoma si salama kwake. Afikirie mahali pengine, lakini si Dodoma,” alisema.

    “Nitumie fursa hii kuwaomba wananchi pale wanapoona mtu wasiyemwelewa au dalili waripoti haraka kwenye vyombo vya habari na dola au kwa viongozi popote pale ambapo wanaweza kushirikiana kuliondoa hilo tatizo. Lakini kwa ujumla hali iko shwari mpaka sasa,” alisema Rugimbana.

     Wakati Rugimbana akisema hayo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Mayalla Towo amesema wameweka miundombinu ya kuweza kuwabaini wahalifu, lakini hawezi kuitaja.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    May kukutana na Merkel Ujerumani

    By: Unknown On: 02:21
  • Share The Gag
  • May amemrithi David Cameron aliyejiuzulu baada ya kura ya maoni
    Waziri mkuu mpya wa Uingereza Theresa May leo amepangiwa kufanya ziara yake ya kwanza ng’ambo kama waziri mkuu ambapo ataelekea mjini Berlin, Ujerumani kukutana na kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
    Viongozi hao wawili watajadili utaratibu wa Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya baada ya raia nchini humo kuidhinisha hatua hiyo kwenye kura ya maoni mwezi uliopita.
    Kadhalika, watajili uhusiano wa kibiashara wa siku zijazo.
    Bi Merkel amekuwa na ushawishi mkubwa Ulaya Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, amesema anatarajia Uingereza kuchukua hatua haraka kumaliza hali ya suitafahamu ambayo imetanda tangu kufanyika kwa kura ya maoni Uingereza.

    Waandishi wa habari wanasema kuanzisha uhusiano wa moja kwa moja baina yake na Bi Merkel litakuwa jambo muhimu sana kwa Bi May anapojaribu kufanikisha mazungumzo ya kuwezesha Uingereza kujiondoa vyema kutoka kwa EU.

    Chanzo BBC

    Wanawe Trump wafana kongamano la Republican

    By: Unknown On: 02:16
  • Share The Gag
  • Donald Trump Jr ana wadhifa mkuu katika shirika la Trump
    Wana wawili wa mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump ni miongoni mwa watu waliohutubu katika kongamano la kitaifa la chama hicho mjini Cleveland, Ohio.
    Kinyume na mkewe Trump, Melania, ambaye alishutumiwa sana alipotoa hotuba siku ya kwanza baada ya kubainika kwamba baadhi ya maneno kwenye hotuba yake yalitoka kwenye hotuba iliyotolewa na mke wa Rais Barack Obama, Michelle, mwaka 2008, wawili hao walisifiwa sana.
    Mwanawe wa kiume, ndiye aliyetangaza kwamba babake alikuwa amepata wajumbe wa kutosha na kuidhinishwa kuwa mgombea rasmi wa chama hicho.
    Hotuba yake pia iliangazia sana sera na sifa za babake.
    “Kwa babangu, lisilowezekana huwa ni mwanzo tu … hivyo ndivyo anavyotazama maisha,” Donald Trump Jr amesema.
    Mwanawe huyo ana wadhifa mkuu katika shirika la Trump Organization na amekuwa mshauri wa karibu wa babake wakati wote wa kampeni.
    Bintiye Donald Trump, Tiffany, pia alimsifu sana babake.
    Tiffany alifuzu hivi majuzi kutoka kwenye Chuo Kikuu cha Pennsylvania na ana wafuasi wengi sana kwenye Instagram.
    Tiffany Trump alifuzu majuzi kutoka chuo kikuu “Amenisaidia sana kuwa mtu bora,” amesema.
    Wengi walimsifu sana kwa kuonekana kutulia, licha ya kwamba alikuwa anahutubia kikao kikuu cha chama.
    Tiffany, 22, ana wafuasi zaidi ya 165,000 kwenye Instagram na ndiye mwana wa pekee wa Donald Trump na mkewe wa pili Marla Maples. Alilelewa Los Angeles, mbali na familia ya Trump.
    Alifanya kazi ya uanamitindo kwa muda na mwaka 2011, alichomoa wimbo kwa jina Like A Bird.
    Donald Trump ana watoto watano, Donald Trump Jr, Ivanka Trump na Eric Trump kutoka kwa mke wa kwanza Ivana Marie Trump, Tiffany Trump kutoka kwa mke wa pili Marla Maples na Barron Trump kutoka kwa mke wa tatu na wa sasa Melania Knauss.
    Ivanka Trump (kushoto) na Donald Trump Jr 

    Chanzo BBC.