Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samiah Hassan Suluhu akisalimiana na viongozi wa dini.
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ina utajiri
mkubwa unaoangaliwa na watu wa mataifa mbalimbali hivyo kuwaomba
viongozi wa dini kuwaombea ili wapate viongozi watakaouangalia utajiri
wa Tanzania kwa ajili ya Watanzania wenyewe.
Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na viongozi wa dini kwa ajili
ya kuwashukuru kwa maombi yao ya kuliombea Taifa wakati wa uchaguzi ili
ufanyike kwa amani na utulivu. Alisema viongozi wa dini waendelee
kuwaombea ili nchi zinazotaka kuigombanisha ili zitumie utajiri wa
Tanzania kujinufaisha, zisipate nafasi na hilo litawezekana kwa kupata
viongozi bora.
“Tanzania ni kwa ajili ya Watanzania, nimeshuhudia katika kampeni
mgodi wa Geita ukiwa na dhahabu ya kutosha lakini vijiji vya jirani ni
maskini wa kutupa. Wanaozunguka wanahangaika na kituo cha afya tu kwa
ajili ya afya zao, tuna kazi kubwa ya kufanya,” alisema.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa PCT, Askofu Yohana Masinga aliiomba
Serikali ya Awamu ya Tano kuongeza ulinzi na usalama wa raia kwani
katika awamu iliyopita kulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani kwa
makanisa kuchomwa moto. Naye Kaimu Shekhe wa Mkoa wa Dodoma, Ahmed Said
alimshukuru Mungu kwa kuuvusha uchaguzi kwa amani na utulivu.
Created by Gazeti la HabariLeo.
Monday, 16 November 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment