Wanajeshi wa
serikali ya Syria, wakisaidiwa na Hezbollah, inaarifiwa kuwa wamesonga
mbele sana dhidi ya wapiganaji, baada ya mashambulio makali ya ndege za
Urusi.
Vyanzo vya wanaharakati na serikali, vinasema kuwa jeshi la
serikali, limekomboa vijiji viwili katika jimbo la Idlib,
kaskazini-magharibi mwa nchi, karibu na barabara kuu inayounganisha miji
mikubwa.Idlib ilikuwa karibu yote imetekwa na ushirika wa wapiganaji, kabla ya Urusi kuingilia kati.
Urusi imefanya mashambulio ya ndege zaidi ya 60 katika saa 24 zilizopita.
Wakati huo huo Rais Vladimir Putin wa Urusi, anatarajiwa kukutana na ndugu wa Mfalme wa Abu Dhabi, kujadili vita vya Syria.
Abu Dhabi inaongoza katika Umoja wa Falme za Kiarabu, yaani Imarati.
Urusi imeingilia kati kijeshi, huku ndege zake zikishambulia wapiganaji kumsaidia Rais Rais Assad.
Na Imarati imo katika ushirika, ambao unalenga wapiganaji wa Islamic State, na inaona ni muhimu Rais Assad aondoke madarakani.
Mkutano huo unafanywa Sochi, Urusi, ambako mashindano ya magari ya kimataifa, yanafanywa hii leo.
Created by BBC SWAHILI



0 comments:
Post a Comment